Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Bw. Geasi Mwaipaja leo amekutana na Asasi zisizo za Serikali ikiwemo Shirika la Reprieve la nchini Uingereza pamoja na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) lengo likiwa ni kupokea kubadilishana mawazo na Asasi hiyo kuhusu marekebisho ya Sheria kuhusu adhabu ya kifo nchini.
Akiongea Katika Kikao hicho kilichofanyika Katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Afisa Programu Mwandamizi kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Bw. Raymond Kanegene amesema, ujio wao umelenga kumtambulisha mwakilishi wa Shirika la Reprieve kwa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania pamoja na kueleza namna gani wamefanya katika nchi nyingine kuhusu kufutwa kwa adhabu ya kifo ya lazima ili kuona kama Tanzania nao wanaweza kurekebisha sheria hiyo ili kuondoa adhabu hiyo.
Amesema kwamba Sheria hiyo imekuwa na changamoto kwa kuwa haitoi uhuru kwa Majaji, katika kutafsiri Sheria, kutoa adhabu mbadala kulingana na kosa lililofanyika na kwa kuzingatia historia au hali ya mtuhumiwa.
Kwa upande wake Afisa programu wa Shirika la Reprieve Bi Linda Kitenge amesema, Shirika hilo llimekuwa kinara kwa kupigania Uhuru wa kuishi kwa kushiriki mijadala mbalimblia inayosaidia kuondoa hukumu ya kifo Katika maeneo mbalimbali ya Afrika yakiwemo Malawi, Kenya na Uganda na sasa limeanza kufanya kazi nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
Alifunga Kikao hicho kwa Niaba ya Katibu wa Tume Bw. Geasi Mwaipaja amesema ni jukumu la Tume kupokea Maoni kutoka kwa wadau mbalimbali na kwamba maoni yao yataendele kufanyiwa kazi kwa manufaa ya Taifa.
Kikao hicho kilihudhuriwa wanasheria Bw. Japhace Tumaini Daud, Afisa Sheria Mwandamizi anayekaimu nafasi ya Naibu Katibu, Kitengo cha Mapitio ya Sheria, Bw. Msafiri Shamsi Idd na Bw. Zakaria Kegoro .
No comments: