Katibu Mtendaji
wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanznaia Griffin Mwakapeje amewataka watumishi
wote wa Tume hiyo ambao hawajapata chanjo ya homa ya inn kutumia nafasi ya Uwepo wa
wataalamu wa afya ofisini hapo kupata chanjo hiyo itakayotolewa kwa muda wa siku
moja ya tarehe 15.08.2023
Akiongea leo baada ya kuwapokea wataalamu hao kutoka Wizara ya Afya nchini ambao
wanatoa chanjo ya Inni kwa gharama za ofisi amesema ni fursa kwa kila Mtumishi
kupata chanjo hiyo kama alikuwa hajapata.
Aidha amesema ili
watumishi waweze kutekeleza majukumu yao vizuri ni lazima wawe na afya nzuri hivyo kila mtumishi anatakiwa kutimiza jukumu hilo kwa kuwaona wataalamu hao.
Huduma hiyo ya
chanjo inapatikana katika ofisi za Tume zilizopo Chuo kikuu cha Dodoma katika
offisi namba 301 ghorofa ya tatu
Awali wataalamu hao
walisema kwamba dalili za ugojwa huo ni Kutapika, kuhara au maumivu ya
tumbo, Rangi ya manjano kwenye macho na ngozi pamoja na mtu kupata choo
kilicho na rangi ya mpauko.
‘Kwa kawaida,
homa kali ya ini inaweza kupona bila hata madhara ya hapo kwa hapo Katika
baadhi ya wagonjwa, maambukizi ya homa kali ya ini aina B au C yanaweza
kusababisha maambukizi sugu na kusababisha kovu, ini kushindwa kufanya kazi au
hata saratani. Homa kali ya ini inakuwa mbaya zaidi kwa watu wazima kuliko
watoto. Watu wazima huonesha zaidi dalili za ugonjwa kuliko watoto na madhara
makubwa zaidi ya ugonjwa huo ni kwa watu wenye umri mkubwa’walisema
No comments: