Menejimenti ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) leo tarehe 15/08/2023 imekutana na baadhi ya wabunge kutoka nchini uganda walikuja kwa lengo la kujifunza sheria ya ndoa inavyotekelezwa hapa nchini.
Akieleza malengo ya ujio wao Mhe. Sarah Opendi Mwenyekiti wa chama cha wabunge wanawake nchini uganda amesema wamekuja kujifunza namna sheria ya ndoa inavyotekelezwa nchini tanzania na changamoto zilizopo kwa sasa na namna wanavyojipanga kuzitatua.
Aidha Mhe. Sarah amesema kwa sasa serikali ya uganda ipo kwenye mchakato wa kuandaa muswada wa sheria ya ndoa hivyo wanalojukumu la kupata uzoefu wa nchi mbalimbali zinazotekeleza sheria hiyo ikiwemo Tanzania na Zimbabwe
Uganda kuna ndoa za aina nyingi ambapo muswada huo unategemewa kugusa jamii yote huku kama ambavyo Tanzania ilivyofanya kwa kuzingatia ndoa za kidini, Ndoa za kimila na Ndoa za serikali ( Bomani)
Kwa upande wake Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Griffin Mwakapeje amesema Tume ina jukumu la kufanya mapitio, utafiti na kutathmini Sheria, eneo la Sheria au mfumo wa sheria husika na kutoa mapendekezo kwa lengo la kufanya maboresho kuiboresha.
Aidha, ameendelea kusema kwamba Tume pia ina jukumu la kutoa elimu ya Sheria kwa umma kwa lengo la kuuwezesha Umma kufahamu mabadiliko na maendeleo yanayotokea katika Sekta ya Sheria.
Akieleza uzoefu kuhusu Sheria ya Ndoa amesema imetambua Ndoa kama taasisi ambayo haina budi kulindwa Kwa lengo la kuwa na Taifa bora. Ni kutokana na hilo sheria inaweka masharti mbalimbali yakiwemo ya mke na mume kuishi pamoja Kwa muda wa uhai wao; aina za ufungaji wa ndoa zinazotambuliwa; nafasi ya mwenza wa ndoa kutoa ridhaa wakati wa kuuza Mali za ndoa; masharti ya talaka; na masharti ya dhana ya Ndoa baada ya wahusika kuishi pamoja bila kuisajili ndoa hiyo.
hata hivyo , Bw. Mwakapeje ametoa maelezo kuhusu uziefu wa Tanzania kuwa Sheria Moja ya Ndoa ilipatikana mwaka 1971 baada ya maridhiano ya wanajamii wote na kuzifuta sheria nyingi zilizokuwepo kama vile Sheria za kimila, kindi, kiislam na za Serikali ambazo zilikuwa zinasimamia masuala ya Ndoa, hivyo Uganda wanaweza kujifunza kwetu ili na wao pia pamoja na mambo mengine waweze kuwa na sheria Moja ya Ndoa tofauti na ilivyo Sasa
No comments: