HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YAPANGA MIKAKATI YA KUTEKELEZA DIRA YA TAIFA 2050





Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) leo tarehe 7 Agosti, 2025 imeeleza namna ilivyojipanga kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 kwa kufanya maboresho katika mifumo ya sheria ili kuhakikisha inakidhi mahitaji ya vizazi vijavyo na kuendana na mabadiliko ya teknolojia, jamii na mazingira duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Naibu Katibu wa Tume hiyo, Bi. Zainab Chanzi, alisema kuwa Dira ya Taifa ya 2050 ni dira pana na ya kipekee inayolenga kuiwezesha Tanzania kuwa Taifa jumuishi lenye ustawi, haki na linalojitegemea.

“Ili Dira ya 2050 iweze kufikiwa, sheria ni nyenzo muhimu katika utekelezaji wa Dira, hivyo sheria zetu lazima ziakisi misingi, nguzo na shabaha za Dira hiyo. Kama Tume, tumejipanga kuhakikisha sheria zinafanyiwa mapitio, tafiti na tathmini na wananchi kuelimishwa maboresho ya sheria kwa lengo la kujenga uelewa kwa wananchi,” alisema Bi. Chanzi.

Aidha Bi. Chanzi alibainisha mikakati mbalimbali ambayo Tume imepanga kutekeleza imiwemo kupitia Sheria zilizopitwa na wakati ili kuhakikisha hazikwamishi maendeleo ya kisasa kama vile matumizi ya akili unde (AI).

Akizungumzia kuhusu sekta ya Kilimo Bi. Zainab alieleza umuhimu wa Sekta ya Kilimo kwa kuwa kwa mujibu wa Dira 2050 ni miongoni wa sekta ya mageuzi hivyo kama Tume imejipanga kuhakikisha sheria zinazosimamia sekta hii zinaakisi matarajio yaliyowekwa na Dira kama vile kuwa Taifa linaloongoza katika uzalishaji wa chakula.


“Sheria tunazotunga leo ndizo zitakazojenga Tanzania ya baadaye. Hivyo basi, kazi yetu ni kuhakikisha msingi huo wa kisheria unawekwa kwa weledi, umakini na mshikamano wa kitaifa,” aliongeza.

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Yatoa Elimu ya Sheria ya Ustawi wa W...

KARIBUNI NANENANE TUWAHUDUMIE

SIKILIZA MAFANIKIO YA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA KATIKA KIPINDI CHA MWAK...

Elimu ya Sheria kwa watanzania ndio Mpango mzima

TAZAMA ELIMU YA MIRATHI ILIYOTOLEWA NA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA MKOANI...


Mwanasheria Vicky Mbunde kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT),Baraka Chipamba, akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kufungua mirathi baada ya marehemu kufariki wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Magomeni Bagamoyo mkoani Pwani Aprili 25, 2025.

 Bagamoyo

Mwanasheria Vicky Mbunde kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), amesema kuandika wosia siyo uchuro bali unasaidia kuondoa migogoro ya kugombea mali zilizoachwa na marehemu.

Hayo yalibainishwa na mwanasheria huyo Aprili 25, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Magomeni mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakati akitoa elimu inayohusu umuhimu wa kuandika Wosia pamoja na kujiepusha na makosa mbalimbali ya kimtandao.

Alisema makosa ya kimtandao yamekuwa yakifanyika kwa kutumia vifaa vya kielektroniki kama kompyuta, simu janja, vishikwambi na Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari (TEHAMA).

Mbunde alisema wosia ni nyaraka ya kisheria ambayo inaonyesha matakwa na maagizo ya mtu kuhusu namna mali yake itakavyogawiwa baada ya kifo chake na kuwa unaweza kujumuisha maelekezo kuhusu jinsi mali itakavyogawiwa kwa warithi, uteuzi wa wasimamizi wa mali, na mambo mengine yanayohusiana na urithi wa mtu husika. 

" Malengo ya kuandika wosia ni kuhakikisha kwamba matakwa ya mtu yatatekelezwa ipasavyo baada ya kifo chake na kuwa unaweza kuwa na athari za kisheria na unaweza kutambulika na mahakama mara tu baada ya kifo cha mtu aliyeandika wosia huo," alisema Mbunde.

Mbunde alisema wosia unaweza kujumuisha mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa warithi na kuonyesha ni nani atakayepokea mali za marehemu.

 Alisema mtu anaweza kuteua watu wa kusimamia mali zake na kutekeleza matakwa yake kama watekelezaji wa wosia ambao unaweza kuainisha jinsi mali inavyopaswa kutumika, kugawanywa, au kuhamishwa kifedha.


 
Mwanasheria wa Tume hiyo, Baraka Chipamba akizungumzia utaratibu wa kufungua mirathi alisema inategemeana kama marehemu aliacha wosia au hakuacha wosia.

 

Alisema kama marehemu aliacha wosia na kumchachagua mtu wa kusimamia na kugawa mirathi yake baada ya yeye kufariki, ataomba mahakamani kuthibitisha wosia huo.

 

Aliongeza kuwa kama hakuna wosia, hatua ya kwanza ni kuchagua msimamizi wa mirathi. ambaye ndugu wa marehemu watalipendekeza jina lake ili asimamie mirathi.

Alisema kazi ya msimamizi wa mirathi ni kufungua Mahakamani shauri la maombi ya kusimamia mirathi, kubainisha, kukusanya na kuhifadhi mali za marehemu, kulipa madeni yaliyoachwa na marehemu na kugawa kilichobaki kwa warithi halali.

 

Chipamba alisema siyo kila mahakama inaweza kusikiliza kesi hizo za mirathi ambapo amezitaja mahakama ambazozinasikiliza mashauri hayo kuwa ni Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya. Mahakama ya Hakimu Mteule na Mahakama Kuu.

 

Alisema unaweza kwenda Mahakama ya Mwanzo kama mirathi inahusisha sheria za Kimila au za Kiislam  na hiyo haijalishi thamani na ukubwa wa mirathi husika hivyo kama wewe ni Mkristo, usiende Mahakama ya Mwanzo na utaenda Mahakama ya Mwanzo iwapo sheria inayotumika kwenye hiyo mirathi ni ya Kimila au Kiislam.

Aidha Chipamba alisema Mahakama ya Wilaya inasikiliza mashauri ya mirathi   ambayo haizidi Sh.100,000,000 kwa hiyo chochote chenye thamani ya kuanzia sifuri mpaka million mia ni  shauri dogo ambalo litasikilizwa.

 

" Usiende Mahakama ya Mwanzo, hata kama mirathi ni fedha ndogo. Utatakiwa kwenda  Mahakama ya iwapo tu sheria inayotumika ni ya kimila au kiislam," alisema Chipamba.

Mwanasheria Vicky Mbunde kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT),Vick Mbunde akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kuandika Wosia kabla ya kifo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Magomeni Bagamoyo mkoani Pwani Aprili 25, 2025.

Mwanasheria Vicky Mbunde kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), Vick Mbunde, akigawa vipeperushi kwa wananchi wa Kata ya Magomeni wilayani Bagamoyo.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Magomeni, Mwajuma Yombe, akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mkazi wa Kata ya Magomeni, Tecra Philipo, akiuliza swali wakati wa utoaji wa elimu hiyo
Walimu wa Shule ya Sekondari ya Hassanali Damji wakishiriki kupata elimu ya sheria kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Dunda, Judith Mayunga, akitoa maelezo wakati wa utoaji wa elimu ya masuala ya mirathi wakati ilipokuwa ikitolewa kwa wafanyabiashara wa Soko la Samaki wilayani Bagamoyo.

Mwanasheria Vicky Mbunde kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), Baraka Chipamba, akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kufungua mirathi kwa wafanyabiashara wa Soko la Samaki Wilaya ya Bagamoyo.
Mwanasheria Vicky Mbunde kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania  (LRCT),Baraka Chipamba, akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kufungua mirathi kwa walimu wa Shule ya Sekondari ya Hassanali Damji.
Wananchi wa Kata ya Magomeni wakipata elimu ya sheria kuhusu mirathi na kuandika wosia.
Elimu ikitolewa.
Mkazi wa Kata ya Magomeni, Seif Chama akiuliza swali.
Maswali yakiulizwa likiwemo matapeli wanawezaje kusajili laini za simu zaidi ya 100 wakati sheria hairuhusu?

Wananchi wa Kata ya  magomeni wakiwa wameshika vipeperushi vya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakati wa upokeaji wa elimu hiyo.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari a Hassanali Damji, Jafari Mwandemo akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Magomeni, Mwajuma Yombe, akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo Shule ya Sekondari ya Hassanali Damji.
Viongozi wakiwa meza kuu wakati wa utoaji wa elimu hiyo Shule ya Sekondari ya Hassanali Damji.
Taswira ya utoaji elimu Shule ya Sekondari ya Hasanali Damji.

 Mkazi wa Kaole Selemani Iddi akiuliza maswali wakati wa mafunzo hayo.