TUME ya
kurekebisha Sheria Tanzania na Ile ya
Zanzibar leo tarehe 12/07/2023 wamesaini Mkataba wenye lengo la
kuboresha utendaji kazi katika tasnia ya sheria ambapo imeelezwa kwamba
ushirikiano huo utasaidia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii Mazingira na
elimu.
Akiongea
kabla ya kusaini mkataba huo Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania
Jaji Msaafu wa Mahakama ya Rufaani Tanzania January Msoffe amesema Tume hizo
zina maono na majukumu yanayofanana hivyo ushirikiano wao utaleta mabadiliko na
tija makubwa.
Alisema kuwa
ushirikiano kati ya Tume hizo utasaidia kuimarisha mfumo wa kisheria
unaozingatia utawala bora na utawala wa sheria kwa maendeleo ya jamii.
"Ushirikiano
huu utakuwa jukwaa muhimu la kubadilishana ujuzi, utaalamu na mbinu bora katika
nyanja ya mageuzi ya sheria katika nchi, tutatumia nguvu zetu ili kuimarisha
utafiti wa kisheria, mapitio na tathmini ya sheria zilizopo na kubainisha
maeneo mbalimbali yenye changamoto na kujitahidi kuondoa upungufu au
mapengo yanayoweza kuwepo kati ya mifumo ya sheria. "Amesema Jaji
Msoffe.
Aidha
amewataka wataalamu wa pande hizo mbili kuhakikisha wanaisoma na kuilelewa
mikataba hiyo ili waweze kuitekeleza
kama inavyostahili ambapo ameeleza kwamba itasaidia kuoboresha utendaji kazi
wao wa kila siku.
Kwa upande
wake Mwenyeki wa Tume ya kurekebisha sheria Zanziba Khadija Shamte Mzee amesema
mkataba huo ni dalili za kukua kwa taasisi hizo kwa kuwa tokea kuanzishwa kwake
hazikuwahi kutokea.
Amezitaka
taasisi hizo kuhakikisha zinabadilisha mitazamo hasi iliyopo kwa baadhi ya watu
kwa kuonesha na kuyatangaza majukumu yao kwa jamii huku akielekeza Tume hizo
kutoa tafiti kwenye shelfu na kuzibainisha kwa jamii kwa kuzifanyia kazi.
Mwenyekiti
huyo ameendelea kueleza kwamba mashirikiano hayo yatapunguza gharama na
uendeshaji wa majukumu ikiwemo utafiti uchapishaji wa majarida na ubadilishaji
wa taarifa mbalimbali.
Ameongeza
kuwa ni wakati wa kuongeza kasi ya utendaji kazi wao kwa kufanya mapitio ya
sheria, kubadilisha mbinu na kuhakikisha
Tafiti zinakuwa ni Mali ya Jamii.
Akielezea
mkataba huo, Katibu Mtendaji wa tume Zanzibar, Mussa Kombo Bakari amesema
mkataba huo una maeneo 10 ambayo ni kuimarisha ushirikiano baina ya tume hizo.
Pia
kubadilishana taarifa ikiwemo ripoti za utafiti na nyaraka, kufanya tafiti
za pamoja, kubadilishana utaalamu na uzoefu baina ya pande zote.
Awali
akieleza majukumu ya tume hizo Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria
Tanzania Griffen Mwakapeje amesema Kazi
ya time hizo ni kufanya mapitio ya Sheria zote za Tanzania na Zanzibar ili ziweze kuendana na Mazingira na jamii
iliyopo.
Hata hivyo
ameendelea kusema kwamba zipo sheria ambazo zinatakiwa kuondolea na kwa kuwa zimekuwa za zamani na zipo ambazo
zinatakiwa kusasishwa na na kufanya mapendekezo ya kutungwa Sheria nyingi
kulingana Mazingira yaliopo.
No comments: