Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Griffin Mwakapeje ameziomba Taasisi mbalimbali Nchini zenye changamoto za Sheria wanazozitekeleza kuleta Maoni kwenyeTume hiyo ziweze kufanyiwa mapitio na utafiti wa kina ili kuepuka maboresho ya Sheria kufanyika mara kwa mara.
Mwakapeje ameyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilichofanyika leo tarehe 22.08.2023 Katika ukumbi wa mikutano Bungeni mjini Dodoma.
Katibu Mtendaji huyo ameendelea kusema kwamba Sheria nyingi zinazofanyiwa marekebisho bila kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria zimekuwa hazifanyiwa utafiti wa kina hivyo kuruhusu mabadiliko ya mara kwa mara hivyo kutoa wito kwa Taasisi zenye changamoto za Sheria kuhakikisha wanazifikisha kwenye Tume hiyo ili ziweze kufanyiwa utafiti wa kina na ziweze kudumu kwa miaka zaidi ya 50 bila kuhitaji mabadiliko.
"Sheria inatungwa January ukifika mwezi Aosti Sheria inahitaji mabadiliko, hii inakuwa si afya katika mfumo wa utungaji wa sheria. Tunataka mtuletee maoni sisi tufanye utafiti wa kina ili sheria zetu zidumu kwa miaka mingi bila kurekebishwa."
Aidha. Mwakapeje amesema ni jukumu la Tume kufanya mapitio na utafiti wa Sheria zote za Jamhuri ya Muungano. Hivyo Kama wataletewa Sheria hizo watazitendea haki kwa kufanya utafiti kina kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Pauline Philipo Gekuli ameipongeza Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kwa kuwa na machapisho mengi ya taarifa za utafiti wa sheria na kuiomba kamati kutilia mkazo mapendekezo yanayotolewa na Tume hiyo kwa kuwa yamefanyika utafiti wa kina.
Mhe. Gekuli ameendelea kusema kwamba umefika wakati serikali kuitumia kikamilifu mapendekezo ya Tume hiyo ili kufunga Sheria zitakazodumu kwa muda mrefu ili kupunguza changamoto kwenye jamii.
Naye Mjumbe wa Kamati ya hiyo Abeid Ighondo Ramadhani Mbunge wa Singida Vijijini amesema Tume ya Kurekebisha Sheria iharakishe ukamilishaji wa mapendekezo ya Sheria ya makosa ya dhidi ya maadili na ifikishwe Bungeni ili tuweze kuiokoa jamii ambayo inaathirika huku akitaka Sheria hiyo itoe adhabu Kali kwa wahusika wa vitendo vya ushoga ili kuondoa tatizo hilo.
No comments: