Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imeanza mazoezi yake kuelekea Mashindano
ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara
za Serikali (SHIMIWI) itakayofanyika mkoani Iringa 27 Septemba 2023 .
Akizungumza jana baada ya mazoezi hayo Katibu Mtendaji
wa Tume ya Kurekebisha Sheria Griffin Mwakapeje amesema wanamategemeo makubwa kwamba timu hiyo
itafanya vizuri katika mashindano hayo.
Aidha Mwakapeje amewataka watumishi
kujenga tabia ya kufanya mazoezi ili kuboresha na kulinda Afya zao na kwamba hata mashindano hayo
yatakapokwisha mazoezi yatandelee kufanyika kila jumanne na alhamisi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Tawi
la SHIMIWI Msafiri Shamsi Idd amesema timu hiyo inaendelea na mazoezi ya michezo
mbalimbali ikiwemo Kuvuta Kamba, riadha, draft,bao na michezo mingine ambayo
inatambuliwa na shirikisho hilo.
Amesema lengo la mazoezi hayo ni
kuhakikisha kwamba Timu ina kuwa na utayari wa kimwili (fitness) pamoja na kujenga
afya jambo ambalo litasaidia Timu hiyo
kutwaa ubingwa wa mashindano watakayoshiriki.
Adha amewataka washiriki wa michezo
mbalimbali kuhakikisha wanafanya mazoezi kila siku ya jumanne na Alhamisi kama
ratiba yao inavyonesha .
No comments: