Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Jaji
Mstaafu January Msofe amewataka watumishi wa Tume hiyo kujipanga na kuhakikisha
wanaendelea kufanya mapitio na utafiti wa sheria zote nchini ili ziweze
kuwanufaisha wananchi
Kauli hiyo ameitoa leo katika ukumbi wa mikutano wa Tume hiyo
uliopo maeneo ya chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alipokutana na watumishi wa Tume
hiyo wakati wa kupata chakula cha mchana pamoja.
“Tume ina jukumu kubwa la kufanyia utafiti sheria zote hapa
nchini na kupeleka mapendekezo sehemu husika hivyo jukumu hili linapaswa kuwa
endelevu na kuonesha tija kwa taifa’ alisema Jaji Msofe.
Jaji Msofe amewataka wanasheria wa Tume hiyo kujipanga
kikamilifu na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ya msingi yatakayosaidia
sheria zinazotungwa kudumu kwa muda mrefu na kuwasaidia wananchi.
Aidha amewataka watumisha hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea
(business as ussual ) badala yake wajikite kufanya utafiti wa kina wa sheria
mbalimbali ili kutimiza msingi wa kuanzishwa kwa Tume hiyo.
“Yapo mapendekezo mbalimbali
kuhusu maboresho ya sheria ya tume ya kurekebisha sheria, sasa ni lazima
tuendelee kufanyia utafiti wa kina sheria mbalimbali kwani serikali inatutegeme,kila
siku hakikisha unakuja na mbinu mpya na
wala tusifanye kazi as business as usual”
alisema jaji Msofe.
Jaji Msofe pia amewataka watumishi wa tume hiyo kuhakikisha
wanashiriki mazoezi ambayo yanafanyika kila siku ya jumatatu na alhamisi ya kila
wiki ili kujenga na kuimarisha afya zao na kuepuka magonjwa nyemelezi.








No comments: