Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania michuoano
ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za
Serikali ( SHIMIWI) inayofanyika Mkoani Iringa baada ya kupata upinzani mkali kutoka timu ya
kuvuta Kamba ya Wizara ya fedha wanaume na Wizara ya Ujenzi wanawake ambapo Tume
ilishindwa michezo yote.
Akiongea leo baada ya kumalizika mchezo Mwalimu wa timu hiyo Bw. Idrisa Juma Shabani
alisema timu zimejithidi lakini bahati haikuwa upande wa Tume na kuwa ni sababu
ya kupoteza mchezo huo.
Idrisa ameendelea kusema kwamba kwasasa
wanajipanga kwa mchezo mwingine wa siku inayofuata huku akitaja kupungukiwa
wachezaji hasa wanawake ambapo kwa mchezo uliopita walilazimika kuvuta Kamba wakiwa
pungufu (9 kwa 10) jambo ambalo ameeleza kwamba limechangia timu ya wanawake
kukosa ushindi.
Hata hivyo amewataka wachezaji kutokata tamaa na
kuendelea kufanya mazoezi ili kuzikabili michezo ya siku inayofuta ambapo
ameeleza kwamba timu za mwaka huu zimejiandaa vizuri.
“tumepoteza michezo yetu miwili baina ya Hazina
na Ujenzi, kwa upande wa wanaume tumeona ki mchezo tulikuwa tumezidiwa lakini
kwa upande wa wanawake walishindwa kwa
sababu walikuwa pungufu, ni imani yangu kwamba kesho tutafanya vizuri zaidi kwa
kuwa tutakuwa tumekamilika sehemu zote.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tumesheria sport
club Msafiri Shamsi Iddi amewataka wachezaji kupata muda wa kupumzika na
kuyafanyia kazi baadhi ya makosa madogo yaliojitokeza na kufuata mafundisho ya
mwalimu ili kuhakisha wanapata ushindi
katika michezo inayofuta.
Akiongea na mwandishi wetu moja ya wachezaji wa tumesheria sport club Azizi Hamisi
Mbuni ambeye pia ni katibu wa Timu hiyo
anasema kushindwa kwa mchezo huo hakuwakatishi tamaa na wanauhakikka kwamba
watafanyia mazoezi maelekezo ya mwalimu na kufanya vizuri katika michezo ijayo.






























No comments: