Bunge lafuta Mapendekezo ya Tumesheria Sport Club - SHIMIWI
2023.
Timu ya kuvuta kamba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
leo imefuta mapendekezo na matarajio ya
timu ya Tumesheria ya kuingia robo fainali Katika mashindano ya Wizara na Idara
za Serikali (SHIMIWI) Katika mchezo wa kuvuta kamba Uliofanyika Katika uwanja
wa Mkwawa Mjini Iringa.
Tume ya Kurekebisha sheria imetolewa na timu ya Bunge kwa
ponti mbili 2-0 ambapo ilivutwa Mara
zote mbili hivyo kupoteza nafasi ya kuendelea na michuano hiyo.
Walipokuwa wakihojiwa wachezaji wa TumeSheria wamesema pamoja na kutumia mbinu
mbalimba za mwalimu lakini walizidiwa
nguvu Katika mchezo huo hivyo wakaupoteza na sasa wanajipanga upya kwa ajili ya
mashindano hayo kwa mwaka kesho.







No comments: