HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

» » MAKAMU WA RAIS AFUNGA MAONESHO YA NNE YA SIDO NJOMBE






Taasisi 30 za Serikali na Sekta binafsi  zilizoshiriki Maadhimisho ya  Nne yaliyoandaliwa na Shirika la  kuhudumia viwanda vidogo (SIDO)  kushiriki kwa nafasi zao Katika uzalishaji wa vifungashio na  kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazokabili  Sekta ya viwanda vidogo na vya Kati  hapa Nchini.


Kauli hiyo imetolewa leo tarehe  28.10.2023 na Makamu wa Ras wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Isdori Mpango wakati wa kufunga maadhimisho hayo yaliyoadhimishwa Katika uwanja wa sabasaba Mkoani njombe baada ya kudumu kwa Siku Sita (6) tokea tarehe 23 yalipofunguliwa.


Makamu wa Rais amesema sekta ya viwanda vidogo na vya Kati Ina mchango mkubwa Katika ukuaji wa uchumi wa nchi hivyo ni muhimu taasisi zisaidie upatikanaji wa mitaji, mazingira mazuri ya biashara , elimu ya ujasiriamali na Sheria mbalimbali zitakazosaidia kupiga hatua mbele.


"Nimetembelea mabanda na nimeona teknolojia mbalimbali za usindikaji na kilimo na nimeskia changamoto mbali mbali zinazokabili Sekta ya viwanda vidogo, hivyo niagize taasisi zote zilizopo hapa kuhakikisha kila moja inatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wajasiriamali"


Aidha Makamu wa Rais ameelekeza Taasisi ya ubora na viwango (TBS) kuhakikisha inawafikia wajasiriamali wadogo ili kuzipatia ubora bidhaa zao huku akizipongeza benki za CRDB, Azania Benki naTADB kwa kupunguza riba kwa wajasiriali wadogo na wakulima.


Hata hivyo, Makamu wa Rais ameagiza gharama za  teknolojia za bidhaa zinazotengenezwa na SIDO  ziweze kupatikana kwa bei nafuu ili ziweze kununuliwa na wajasiriamali wadogo na wakati na zipatikane sehemu mbalimbali Nchini.


Awali Mkuu wa Mkoa huo Antony Mtaka amesema maonesho hayo yamehusisha wajasiriamali 628 Kati ya 800 waliokuwa wametakiwa na Taasisi 30 za Serikali na Sekta Binafsi.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Tuandikie Maoni yako