Timu ya riadha ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imefuzu kwenda hatua ya robo fainali katika
mchezo huo baada ya kushika nafasi ya tatu Katika mbio za urefu wa Mita 200 ambao umefanyika leo Katika uwanja wa
Samora uliopo mjini Iringa ikiwa ni mashindano ya Wizara na Idara za Serikali
(SHIMIWI)
Akiongea baada ya
mchezo huo Mwenyekiti wa timu ya
Tumesheria Bw. Msafiri Shamsi Iddi amesema nafasi hiyo imechukuliwa na mchezaji
Respicious Rweymamu Kashero baada ya kupita washindani wake nane kutoka wizara
na Taasisi mbalimbali waliokuwa wakishiriki mchezo huo.
Aidha ameeleza kwamba Kashero atashiriki mbio hizo kwa mara nyingine mnano siku ya
kesho tarehe 6/10/2023 kwa ajili ya
mchezo wa nusu fainali ambao utakuwa ni mtoano.
Mwanyekiti huyo amesema
mchezo huo ni muhimu kwa kuwa ndio utakaosabaisha tumesheria kusonga mbele Katika mchezo wa riadha au kutolewa kwenye mashindano hayo.
Hata hivyo Msafiri ameendelea kusema kwamba wachezaji wengine walioshiriki mchezo
huo ni Zakaria Kegoro ambaye alishiriki
mbio za Mita 100 na kushika nafasi ya
tano (5) huku mkimbiaji mwingine Emmanuel masamu akishiriki mbio za urefu wa Mita Mia nne(400)
ambapo hakuweza kumaliza baada ya kupata maumivu kwenye misuli.
Msafiri alieleza kwamba mwanariadha Bw. Emanuel Aidani Kayumbo ambaye alishiriki
mbio mita 100 za wazee wa umri wa miaka kuanzia 55 ambapo alishika nafasi ya
saba (7) baada ya kuanguka na kupata majeraha katika mguu wake wa kulia.
Katika hatua nyingine Timu ya kamba ya Tumesheria Sport Club
inatarajia kuingia uwanjani kupambana na timu ya Bunge Siku ya Ijumaa tarehe
6/10/2023 ikiwa ni hatua za mtoano.









No comments: