Wajumbe wa baraza la wafanyakazi la Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania
(LRCT) wametakiwa kutimiza wajibu wao wa
kushughulikia mipango ya Taasisi hiyo (planning ) utunzaji wa mali au bidhaa na
kupokea au kujadili taarifa ya mapato na matumizi (budget) badala ya kutumia
muda mwingi kulalamika au kukosoa viongozi huku wakikumbushwa kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa huo wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichofanyika tarehe 18.10.2023 katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kigoma ambapo ameeleza kwamba
mikutano hiyo isitumike kama uwanja wa fujo kwa kulalamika au kukosoa viongozi
pasipo kuwa na tija.
“Mada kuhusu Wajibu wa Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi ambayo
itawasilishwa na Afisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu), ni muhimu sana kwani ikumbukwe kuwa bila kujua wajibu wao,
wajumbe wanaweza kudhani kuwa jukumu lao kubwa ndani ya Baraza ni kulalamika,
kulaumu, kushutumu, kukosoa na mambo
mengine kama hayo hivyo, kufanya mikutano ya mabaraza iwe ni uwanja wa fujo
badala ya kuwa mahala pa kushirikishana katika kujenga Tume yetu.” Alisema DC
Salum.
Aidha DC Salum alibainisha kwamba Baraza hilo lina dhima kubwa katika maendeleo ya taasisi
hivyo kuwataka wajumbe kuhakikisha wanajua
majukumu yao ili kuwatendea haki watu
wanaowawakilisha.
“kuingia katika Baraza bila kujua jukumu lako la msingi ni sawa na wizi
kama wizi wa aina nyingine hivyo kama mjumbe, utakuwa huwatendei haki
wafanyakazi wenzako unaowawakilisha” alisema
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Katibu wa Tume hiyo Bw. Burhani Kishenyi
amesema Mada mbalimbali zitajadailiwa ikiwemo taarifa ya Mabadiliko yaliyotokana
na Maberosho Mbalimbali ya Kisera na Kisheria yaliyofanyika katika Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya.
Mada nyingine ni kuhusu Taarifa ya Utekelezaji kwa mwaka
wa fedha 2022/2023 yaani kuanzia Julai, 2022 hadi Juni, 2023. Itakayojumuisha
Mipango, Vipaumbele na Bajeti ya Tume katika mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo
amesema ni muhimu kwa ustawi wa Tume kwakuwa itasaidia kujitathmini katika
utekelezaji wa majukumu ili kujua mafanikio, changamoto na sababu za changamoto
hizo.
“Niseme wazi kuwa, mada hii ndiyo sababu ya msingi ya
kufanyika kwa mikutano ya Mabaraza ya Wafanyakazi, ili kujua tulikotoka, tulipo
na tunakokwenda kama Taasisi, kila mjumbe azingatie kikamilifu mada husika. Alisema
Kishenyi
Hata hivyo Kishenyi alieleza kwamba Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania
katika mwaka huo wa fedha ilipata Tsh Bilioni 4.66 ambapo milioni 730 ni mishara na Tsh. Bilioni tatu (3) ilikuwa kwa matumizi
mengine.






No comments: