Wadau wa Sheria wanaoendelea kutembelea Banda la Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania katika maonesho ya wiki ya sheria nchini yalioanza 24 januari 2024 katika viwanja vya Nyerere Square Mkoani Dodoma, wameomba Tume hiyo kuendeleza huduma ya utoaji wa elimu vijijinikwakua wananchiwa maeneo hayowana uhitaji wa elimu ya sheria.
Akizungumza 25 januari 2024 alipofika katika Banda la Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) moja yamwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Bw, Peter Clemence Ndwewe (57) amesema Pamoja na Tume hiyo kuendelea kutoa elimu kupitia maonesho na vyombo mbalimbali vya Habari bado wananchi wanauhitaji mkubwa wa msaada wa elimuya kisheria na wanashindwa kupata huduma hiyo kutokana na tasisi nyingi kuwa zinapatikana mijini.
“Tunawaomba haya mambo yasiishie mijini tu myalete kule vijijini, Tume ya kurekebisha sheria muje kuelimisha vijijini wananchi wajue sheria na haki zao” alisema Bw. Peter.
Nae Abuswamad Othman ambae ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo cha Mipango anayesomea kozi ya maendeleo ya jamii ameishukuru Tume hiyo kwa mipango yake ya utoaji elimu kwa jamii kwani anaona kuna umuhimu mkubwa wa kuimarisha mashirikiano kati ya Maafisa maendeleo ya jamii na maafisa wa Tume hiyo kwakua changamoto zinazozikumba jamii kama vile ukatili kwa Watoto na unyanyasaji kwa akina mama hutokana na kutojua sheria kwa jamii hivyo ushirikiano utarahisisha kufikishia jamii elimu kwa urahisi.
Akijibu kuhusu hali ya utoaji elimu Afisa sheria wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania Respicius Rweyemamu alisema, licha ya maonesho hayo yanayoendelea katika kipindi hiki cha wiki ya sheria lakini Tume hiyo imekua na utaratibu wa kutoa elimu kupitia vyombo vya Habari redio, televisheni na magazeti ambapo ameeleza wamekua wakitumia njia hiyo ili kuwafikia wananchi wengi kwa muda mfupi.
Aidha Rweyemamu ameongeza kuwa Tume imekua ikitoa elimu hata kwa njia ya mikutano kwenye vijiji, kata wilaya na mikoa na wakati mwingine haupita katika taasisi, mashirika na ofisi mbali kwa ajili ya kutekeleza jukumu hilo la utoaji elimu, kuchukua maoni na mapendekezo mbali mbali ya wananchi juu ya mabadiliko ya sheria nchini.
“Hatuwezi kuishia hapa kutoa elimu sisi kama Tume tunao utarataibu wa kutoa elimu na tumekua tukiutekeleza kupitia vyombo vya habari na hata ana kwa ana kupita katika mikoa, wilaya, kata mpaka vijiji pia kuzipitia tasisi na mashirika kutoa elimu na kuchukua maoni yao kwahiyo tunaendelea na tutaendelea na jukumu hilo ili jamii ipate uelewa” alisema Rweyemamu.
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania inashiriki katika maonesho ya wiki ya Sheria kitaifa mkoani Dodoma ambapo yanatarajiwa kufika tamati 30 Jan 2024 na kilele kufanyika Februari Mosi mwaka huu katika viwanja vya chinangali Park mkoani humo.







No comments: