Watumishi Tume ya Kurekebisha
sheria Tanzania wamehimizwa kuwahudumia wananchi ipasavyo ili kuwasaidia kuwa
na uelewa juu ya masualala mbali mbali ya kisheria.
Rai hiyo imetolewa 26 januari
2024 na aliewahi kuwa katibu mtedaji Tume ya kurekebisha sheria Tanzania
2008-2011 Bw. Japhet Mojelwa Sagash alipotembelea banda la Tume hiyo katika
maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square Mkoani
Dodoma.
Bw. Sagash alismea jamii
inauhitaji wa huduma za kisheria na kwakua miongoni mwa majukumu ya tume hiyo
ni kutoa elimu na kuchukua maoni ya wananchi na wadau hivyo iendelee na kasi ya
kuwafikia wananchi ili kuwapa elimu ya kisheria.
“wafayakazi wa hii Tume
nawahimiza wawafuate wananchi na wale wananchi wenye ufahamu juu ya tume nao
waje kutoa maoni yao wasikae kusubiri kufuatwa” alisema Sagash.
Aidha katika hatua nyingine Mstaafu huyo ameiomba wizara ya katiba na
sheria kuitengea bajeti toshelezi Tume hiyo ili kuipa nguvu ya kuweza kufika
sehemu zote za nchi kutekeleza jukumu la utoaji elimu ya sheria kwa umma.
“Naiomba Serikali kupitia wizara
yetu ya katiba na sheria hii Tume ipewe kiasi cha Fedha cha kutosha kwa sababu
kazi ya hii Tume ni utafiti wanatakiwa kuzunguka kila mahali hivyo lazima wawe
na pesa ili wafike katika hayo maeneo wasipokua na pesa inakua vigumu
kufanikiwa kuwafikia watu maeneo mbali mbali” alisisitiza Sagash








No comments: