Tume
ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) na Tume ya Kurekebisha Sheria ya Zanzibar
leo tarehe 11/03/2024 zimekutana katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Tume ya
Kurekebisha Sheria Zanzibar kwa lengo la kujadiliana namna ya kuimarisha
ushirikiano wao katika kazi za mapitio na utafiti wa sheria mbalimbali za
Muungano hasa zinazosimamia mambo ya maadili ili kupunguza kadhia ya ukosefu wa
maadili katika jamii
Akiongea
katika kikao kazi hicho Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Bw. George
Mandepo alisema kikao hicho kinalenga kuimarisha uhusiano baina yao katika utafiti na mapitio ya sheria na
kimelenga kuongeza wigo wa kufanya mapitio ya sheria zinazosimamia maadili.
Aidha
Mandepo ameeleza kwamba katika kikao hicho wameadhimia uwepo wa mafunzo ya
pamoja ya ndani na nje ya nchi kama sehemu ya kuwajengea uwezo watumishi wa
Tume hizo ikilinganishwa na hali ilivyo sasa ambapo kila upande ulikuwa na
utaratibu wa tofauti wa kuwajengea uwezo watumishi.
“
tumekubaliana mambo mengi ya msingi moja wapo ikiwa ni kuandaa na kushiriki
mafunzo ya pamoja ya ndani na nje ya nchi kwa watumishi wetu ili kuwajengea
uwezo” alieleza Mandepo.
Aidha
Bw. Mandepo ameeleza umuhimu wa kutumia mifumo ya TEHAMA katika kuweka na
kusambaza taarifa muhimu za Tume hizo ili kuwafikia wadau wengi kwa wakati huku
akibainisha kwamba wamekubaliana kufanya vikao vya mara kwa mara ambavyo
vitasaidia kuongeza ufanisi.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Bw. Musa Kombo
Bakari akitoa shukrani zake ameishukuru LRCT ambapo ameeleza kwamba kikao hicho
kimetoa mwanga hasa katika kipindi hiki ambacho wanaendelea na mapitio ya
sheria zinazosimamia mambo ya maadili ambapo kwa Tanzania bara walikuwa
wameshapiga hatua katika ukamilishaji wa
kazi hiyo.
Hata
Hivyo Bw. Kombo ameendelea kueleza umuhimu
wa mashirikiano hayo ambayo yatasaidia kubadilishana
uzoefu wa kazi na kupata mawazo mapya hasa wakati huu ambao wapo katika
hatua mbalimbali za kutafsiri sheria kwa lugha ya Kiswahili.
“kukutana
kwetu leo kumetuongezea kitu,hili linadhihirisha kwamba tutakavyokuwa tunakutana
kutasaidia kupata mawazo mapya ambayo yatakuwa ni chachu kwenye kazi zetu”
Kombo alimalizia.
mwisho






No comments: