Tume ya Kurekebisha
Sheria Tanzania imetakiwa kuangalia upya
sheria za usafiri ardhini kwa kuzifanyia mapitio na utafiti wa kina kwa kuwa
zimeonekana kutodhibiti kikamilifu ajali
za barabarani ili ziweze kuwalazimisha
wamiliki wa vyombo hivyo kuimarisha
huduma na kuwapunguzia kazi madereva kwa kuendesha mwendo mrefu kama hatua za
kupunguza ajali za barabarani.
Maelekezo hayo
yametolewa leo tarehe 03/06/2024 na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Pindi Chana
wakati akifungua kikao kazi cha Kamisheni ya Tume hiyo ambacho kimefanyika Mkoani Morogoro
katika hoteli ya Morena kwa ajili ya kupitia taarifa saba (7) za utafiti uliofanywa
hivi karibuni.
Waziri huyo ameeleza
kwamba imekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa
wananchi kupoteza maisha na kupata ulemavu wa kudumu unaosababishwa na ajali za
barabarani zinazotokana na makosa yanayoweza kuzuilika hasa kwa mabasi yaendayo
masafa marefu.
“Umefika wakati Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kufanya utafiti na kuja na
mapendekezo madhubuti yatakayosaidia
kuondoa ajali za barabarani ili kulinda afya na maisha ya watanzania kwa
kuwalazimisha wamiliki kuajiri dereva zaidi ya mmoja katika chombo kimoja cha
masafa marefu” alisema Waziri
Aidha ameagiza
Tume hiyo kushirikiana na wasimamizi wa sheria ya barabarani ili kutafuta suluhisho la kudumu la kuwalinda
wasafiri kwa usalama na kuhakikisha
wanafika kwa wakati, huku akiligusia swala la bima za maisha katika kuwasidia
wathirika.
“Sisi kama wabobevu wa
sheria lazima tuangalie kama kampuni inapata ajali za mara kwa mara waachane na
biashara ya kusafirisha watu na badala yake wasafirishe mizigo.” alisema
Aidha ameendelea kueleza kwamba Tume ya
Kurekebisha sheria kupitia wizara ya katiba na sheria ambao ndio wenye dhamanahazipotayari
kuona tayari kuona wananchi wakipoteza maisha kila kukicha.
Aidha, ameitaka Tume ya
kurekebisha sheria wasisubiri kuletewa kazi za utafiti au mapitio kama ilivyo sasa na badala yake wafanye
kulingana na wanavyoona hali halisi na wanayoyapata wakati wa utafiti.
Hata hivyo Mhe. Waziri aleeza kufarijika kwake na utekelezaji
wa mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai yanayofanywa na Tume hiyo ambazo ni Taarifa ya Mapitio ya Mfumo wa
Sheria Zinazosimamia Makosa ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa Nchini; Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Kifungu cha
91(3) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai;
Utekelezaji mwingi umekuwa
katika Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Mashahidi na
Watoa Taarifa; Taarifa ya Mapitio ya
Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Dhamana; na Taarifa ya Mapitio ya Sheria Zinazosimamia
Adhabu ya Viboko Mahakamani na Katika Magereza.
Awali akimkaribisha Waziri huyo Jaji
wa Mahakama ya Rufani, Winfrida
Beatrice Korosso, ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania,
alieleza kwamba Kikao cha Kamisheni ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ni
Kikao cha 94 toka Tume hii kuanzishwa ambapo Tume , inatekeleza wajibu wake
ipasavyo kwa kuhakikisha vikao vyote vya Kisheria vinafanyika hususan baada ya utafiti na mapitio ya
kitaaluma.
Aidha alieleza
kwamba Taarifa zilizokamilishwa na Sekretariati, ya Tume baada ya kufanyika Mapitio, Utafiti na
Tathmini katika nyanja mbalimbali za
sheria ni Taarifa ya
Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa
Nchini na Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Kifungu cha 91(3) cha Sheria ya
Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Kuhusu Uondoshaji wa Mashauri Mahakamani.
Pia taarifa
ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Mashahidi na Watoa Taarifa;Taarifa
ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria Zinazosimamia Usafiri Ardhini; Taarifa ya
Mapito ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Dhamana; Taarifa ya Mapitio ya Sheria
Zinazosimamia Adhabu ya Viboko Mahakamani na Magereza;naTaarifa ya Tathmini ya
Utekelezaji wa Sheria Zinazosimamia Hakimiliki na Hakishiriki.
Mwisho
No comments: