Tume
ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) imefanya ziara katika Mikoa ya Manyara,
Arusha na Kilimanjaro kwa lengo la kutoa
elimu ya sheria mbalimbali kwa wananchi
Ziara hiyo ilibainisha kwamba Sheria ya “plea
bargaining” imeleta mwamko mkubwa miongoni mwa wakazi wa Mkoa wa Arusha na
kwingineko Tanzania kutokana na manufaa yake ya kupunguza muda wa kesi, gharama
za uendeshaji wa mashauri, na hata kuepuka msongamano katika magereza.
Hayo ni baadhi mambo ambayo wananchi mkoani
Arusha walizungumza kwa njia ya simu na ujumbe mfupi wa maneno katika kituo cha Redio cha TBC na Savvy Fm wakati Wanasheria
wa Tume hiyo Vick Mbunde na Anjela Shila wakitoa elimu ya sheria kuhusu kupunguziwa adhabu kwa kukiri kosa.
Awali akifafanua kuhusu sheria hiyo Wakili wa
Serikali Vicky Mbunde alisema kwamba Plea bargaining, inayojulikana pia kama makubaliano ya
kukiri kosa kwa makubaliano maalum, sheria ambayo ilianza kutumika rasmi
Tanzania kupitia mabadiliko ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) ya
mwaka 2019, na imekuwa ikihamasishwa kwa nguvu katika mfumo wa sheria.
“mtuhumiwa
anapokiri kosa mbele ya muendesha mashtaka , anaweza kupunguziwa adhabu baada yay
a mahakama kujiriidhisha na alichokiri . Huu ni utaratibu unaotambuliwa
kisheria kama "plea bargaining" ambapo mahakama inaweza kuzingatia
kukiri huku kama sababu ya kupunguza adhabu”. Alisema Wakili Vicky Mbunde.
Katika
kipindi hicho ambacho wananchi wengi walipiga simu na kutuma ujumbe ,fupi waliuliza
idadi kubwa ya maswali huku wakitwataka mawakili hao wa serikali kufafanua
umuhimu wa kukikri kosa kwa m,mtuhumiwa na upande wa serikali.
Akiji maswali hayo wakili Anjela
shila alifafanua kwamba sheria ya Plea Bargaining ina umuhimu mkobwa kwa wananchi na serikali
kwa ujumla kwa sababu inaharakisha Utaratibu wa Kesi Mahakamani kutokana na idadi kubwa ya kesi zinazojazana kwenye
mahakama za ngazi tofauti hivyo , mfumo wa plea bargaining umeonekana kuwa
mkombozi kwa kuwa unaruhusu kesi kumalizwa haraka bila kupitia mchakato mrefu
wa usikilizaji.
Hata hivyo Wakili Anjela
amefafanua kwamba mfumo huo unasaidia kupunguza
Msongamano wa Magereza
kwa maana kwamba kuna nafasi ya kuangalia mashauri yao kwa mtazamo mpya, wakati
mwingine kupokea adhabu nyepesi kwa kukiri mapema na kupunguza athari za kifungo
kirefu bila ulazima ambapo alieleza kwamba mfumo huu pia unahimiza wahusika
kubadilika na kujifunza kutoka kwenye makosa bila adhabu kali zisizo za lazima.
Aidha alieleza kwamba mfumo huo
unasaidia kukuza Uwajibikaji na Haki ambapo Kupitia plea bargaining,
mahakama na waendesha mashitaka wanaweza kutoa nafasi kwa washtakiwa ambao wako
tayari kukiri kosa na kushirikiana na vyombo vya dola kwa uwazi ambao ambalo
limeelezewa kwamba linachochea utamaduni wa kuwajibika na kuleta ustawi kwa
jamii kwa ujumla.
Hata hivyo Anjela Shila aliongeza
kwamba mfumo huo wa sheria una manufaa kwa Wakati wa Uchumi Mgumu ambapo kutokana na changamoto za
kiuchumi, plea bargaining imekuwa muhimu kwa kuwa inapunguza gharama kwa pande
zote.
Alieleza
kwamba serikali inapunguza gharama za uendeshaji wa kesi ndefu, na kwa washtakiwa,
wanapunguza muda wa kutumia kwenye kesi na kufungua nafasi ya kuendelea na
shughuli za kiuchumi.
Kulingana
na ujumbe na simu zilizokuwa zikipokelewa katika vituo hoivyo vya Redio
vinadhibitisha kwamba Wakazi wa Arusha wameanza kuelewa kuwa mfumo huo unaweza
kusaidia kupunguza muda wanaotumia mahakamani, jambo ambalo limepunguza shaka
na kuleta matumaini kwa wale waliokuwa wakisubiri mashauri yao kwa muda mrefu.
No comments: