Mwejikiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Jaji Winifrida Korosso akimkabidhi Taarifa nane (8) waziri wa katiba na Sheria Prof. Paramagamba Kabudi katika mkutano uliofanyika jana tarehe 16/10/2024 katika ukumbi wa wizara hiyo uliopo Mji wa Serikali Mtumba
Tume ya
Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) imeshauriwa kufanya mageuzi ya kimuundo na
kuwa Taasisi ya utafiti inayojitegemea ambayo itakuwa chanzo cha fikra za kisheria cha serikali (think Tank) kama zilivyo taasisi
nyingine za utafiti hapa nchini ili kuipatia uwezo mkubwa wa kufanya tafiti na kutoa mapendekezo thabiti
kwa ajili ya marekebisho ya sheria.
Ushauri huo
umetolewa leo tarehe 16/10/2024 na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Paramagamba
Kabudi wakati wa mkutano wake wa kupokea taarifa nane (8) za utafiti kutoka kwa tume
hiyo, Makabidhiano yaliyofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo ulioko mji wa serikali Mtumba.
Prof Kabudi
amesema kwamba kuifanya Tume ya Kurekebisha Sheria kuwa
taasisi ya utafiti inayojitegemea kutaisaidia
kuongeza uwezo wa taasis katika kuboresha ufanisi na kuimarisha kazi zake.
Aidha
ameeleza kwamba mageuzi ya kimuundo yanayoshauriwa
yanakusudia kuhakikisha kuwa Tume hiyo inapata uhuru zaidi wa kufanya tafiti za kina juu ya
sheria, na hivyo kutoa mapendekezo ya maboresho ya sheria kwa uhuru zaidi bila
kuingiliwa na mamlaka nyingine.
“Ikiwa Tume hii itakuwa taasisi huru ya utafiti, itakuwa kama taasisi
nyingine za utafiti ambazo zinafanya kazi za kitaaluma na kutoa ripoti zilizo
kamili na za kina kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria”. Alisema Prof. Kabudi.
Aidha,
amesisitiza Tume hiyo kuanza kujiandaa kwa kuwasomesha wataalamu wake wa
utafiti wa sheria ili waweze kuwa na elimu kuanzia ngazi ya uzamili na
kuendelea ikiwa ni pamoja na kufuatalia kwa ukaribu maslahi yaliyobora kwa
makamshna pamoja na watumishi wote kwa
ujumla.
Mageuzi haya yanaweza pia
kuiwezesha Tume kuanzisha miradi ya utafiti yenye msukumo wa kitaaluma na
inayoweza kuchangia katika maendeleo ya mfumo wa sheria nchini kwa ujumla.
No comments: