Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) imetoa elimu kuhusu dhana ya mapato yatokanayo na uhalifu, ambayo inahusu mali, fedha, au faida zinazopatikana kutokana na vitendo vya kihalifu.
Wakitoa mada hiyo katika kituo cha redio cha Banana
Fm na Redio five ya Mkoani moshi na Arusha Mawakili
wa Serikali Anjela Mnzava Shila na Vicky
Mbunde kutoka Tume hiyo wamesema lengo la elimu hiyo ni kuhakikisha jamii
inaelewa kuwa mali zote zinazopatikana kupitia njia zisizo halali zinaweza
kuchukuliwa na serikali kupitia taratibu za kisheria ili kudhibiti uhalifu na
kupunguza motisha kwa wananchi wa kushiriki katika vitendo vya kihalifu.
Wakili wa serikali Anjela Shilla akielezea
maana ya mapato ya uhalifu alisema ni mapato au mali yoyote itokanayo na
uhalifu ambapo alibainisha kwamba suala
la mapato yatokanayo na uhalifu ni mtambuka kwa kuwa linalogusa sheria mbalimbali kama vile Sheria
ya Mapato Yatokanayo na Uhalifu, Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ,
Sheria ya Kuzuia Utakasishaji wa Fesha Haramu, Sheria ya Kudhibiti na Kupambana
na Dawa za Kulevya, Sheria ya Wanyamapori, na Sheria ya Kuzuia Usafirishaji
Haramu wa Binadamu. Sheria hizi zimeelezea namna ya utaifishaji wa mali
zitokanazo na uhalifu kwa Nia ya kuzuia uhalifu na kufundisha jamii kuwa
uhalifu haulipi.
Aidha Shila ameeleza kwamba elimu hiyo inahusisha kuwaelimisha wananchi na
taasisi za fedha juu ya mbinu zinazotumika kuficha mazao ya uhalifu, kama vile
utakatishaji wa fedha, na umuhimu wa kutoa taarifa wanapoona shughuli za
kutiliwa shaka.
Kwa upande
wake Wakili Vicky Mbunde amefafanua
kwamba zipo sheria ambazo zinazohusika na kusimamia mapato yatokanayo na
uhalifu ambazo zinalenga kudhibiti, kuchunguza, na kutaifisha mali au fedha
zinazopatikana kupitia vitendo vya kihalifu.
Tanzania kama nchi mwanachama wa mikataba
mbalimbali ya nje ya nchi imesaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa Dhidi ya Uhalifu
wa Kupangwa Unaovuka Mipaka na Mkataba wa Umoja wa Mataifa Dhidi ya Rushwa
unaotaka nchi wanachama kuweka Mifumo dhabiti ya kisheria ya Kupambana na
Uhalifu








No comments: