Matumizi ya lugha ya kiswahili katika
kutafsiri sheria za Tanzania yataongeza uelewa kwa wananchi na kuwasaidia kujua
haki na wajibu wao katika utatuzi wa migogoro mbalimbali inayowakabili na kuongeza
utii wa sheria bila shuruti.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji
wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Griffin Mwakapeje wakati akitoa
wasilisho kuhusu mchango wa lugha ya kiswahili katika upatikanaji wa haki
wakati wa kongamano lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Mount
Meru iliyopo jijini Arusha.
Katibu huyo ameendelea kusema kwamba
matumizi ya lugha ya kingereza badala ya lugha ya kiswahili kinachoeleweka na
kutumiwa na wananchi wengi inawanyima kufahamu na kuelewa sheria mbalimbali.
Aidha Mwakapeje ameliomba Baraza la Kiswahili la
Taifa (BAKITA) kuendelea na utafiti ili kupata misamiati muhimu itakayotumika
katika sheria ili kuwaondolea ukakasi mahakimu na majaji kwa kuwa wanapata
ugumu katika kuandika hukumu kwa lugha ya Kiswahili.
Bw. Mwakapeje amebainisha kwamba
kwa sasa Tume ya Kurekebisha Sheria ipo katika utekelezaji wa jukumu la
kutafsiri sheria na ripoti mabalimbali za kisheria kutoka lugha ya kingereza kwenda lugha ya Kiswahili
ili kuisaidia jamii kupata uelewa wa sheria hizo.
“ sisi tunapokwenda kutoa elimu kwa wananchi tunaona hitaji la sheria na
machapisho mbalimbali kuwa kwa lugha ya Kiswahili ili kuwasaida kufanya rejea
mbalimbali” Mwakapeje
Amesema pia Tanzania ina jumla ya
sheria 550 ambapo kati ya hizo zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ni 246
ambapo bado juhudi zinaendelea kukamilisha zoezi hilo.
“ unaweza kuona sheria zilizotafsiriwa ni zaidi ya nusu lakini
tumejipanga kuhakikisha kwamba zeezi linakamilika kwa wakati” Griffin
Mwakapeje.
No comments: