Serikali imesema itaendelea kuimarisha na kutoa ushirikiano kwa
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ili kuimarisha utafiti wa sheria mbalimbali hasa kipindi
hiki ambacho Serikali imeamua kupeleka msaada wa kisheria kwa jamii.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Wizara ya Katiba na
Sheria Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa kufungua kongamano la huduma za msaada wa
kisheria uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Mount Meru iliyopo mjini
Arusha ambapo amesema msaada wa kisheria
unakwenda sambamba na utafiti wa sheria .
Dkt.Ndumbaro Amesema utafiti wa sheria ni muhimu kwa kuwa
ndio unaotathmini ubora na uhalisia wa sheria kwa jamii jambo ambalo ameipongeza
Tume ya kurekebisha sheria Tanzania kwa
namna wanavyokusanya maoni na wanavyopeleka elimu kwa wananchi.
Hata hivyo ameitaka Wizara ya Katiba na Sheria kuimarisha
ushirikiano baina yao na Tume pamoja na
wadau wengine wa sheria kwa kuwa sekta
hiyo ni ya zamani lakini bado ni changa na inahitaji ushirikiano mkubwa.
Aidha Ndumbaro ameeleza kwamba ni muhimu Wizara yake kuongeza ushirikiano baina ya Tume hiyo pamoja
na wadau wengine ili kuweza kufanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na wadau
mbalimbali.
Aidha Ndumbaro ameeleza kwamba ushirikiano huo umesaidia
katika utekelezaji wa kampeni ya msaada wa sheria “Mama Samia legal Aid campaign”
iliyofanyika katika mikoa minne (4) ya Ruvuma,Tabora na Dodoma ambapo jumla ya
watu 255,397 sawa na watu 62,000 kwa kila mkoa walifikiwa na kupatiwa huduma.
Hata hivyo ameelekeza kufanyika kwa tafakuri ili kubaini changamoto zilizotokea wakati
wa utekelezaji wa kampeni kwa awamu ya kwanza ya utoaji wa huduma ya kisheria katika mikoa hiyo ili kuleta urahisi katika utekelezaji wa
huduma hiyo kwa awamu ya pili.
Katika hatua nyingine Dkt. Ndumbaro ametumia mkutano huo
kutoa msimamo wa serikali juu ya kukamatwa
kwa Dkt. Slaa (Balozi) na wenzake watatu ambao wanashikiliwa na jeshi la polisi
kwa tuhuma kwamba wametumia vibaya uhuru
wao wa kujieleza na kufanya uchochezi pamoja na uhaini kwa kuitisha maandamano
na kutoa kauli za vitisho dhidi ya Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Waziri huyo ameeleza kwamba serikali haiwezi kumfumbia mtu
macho akatoa lugha zenye kugawa watu na kuhamasha vurugu kwenye nchi
inayoendeshwa ki katiba na sheria na akaachiwa aendelee kuvunja amani badala
yake atafikishwa mahakamani ili mahakama iweze kutoa maamuzi yake kulingana na walichokifanya
huku akiwataka wanawatetea wajipange kwenda kutoa ushahidi mahakamani.
Hata hivyo aliendelea kusema kwamba hakuna uhusiano kati ya mkataba
wa Bandari na kukamatwa kwao kwa kuwa wapo watu wengi watu wengi waliotoa maoni
yao kwa nyakati tofauti na hawakukamatwa, kwa kuwa hawakuvunja sheria wakati wa
kutuoa maoni yao.
Aidha Ndumbaro amezionya Taasisi za Kimataifa ambazo zinatoa
kauli zenye sura ya kulichafua taifa kuhusu swala hilo na kuwataka kuacha mara
moja kwa kuwa nchi hii inaendeshwa kwa kufuata katiba na kisheria.
Mwisho
No comments: