Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania imeanza ujenzi wa mfumo wa
kielektroniki wa utendaji kazi za Mapitio, Tathmini, na Utafiti wa Sheria
mbalimbali za Tanzania bara utakarahisisha utekelezaji wa majukumu, kupunguza
gharama, na kuboresha utunzaji wa kumbukumbu
za nyaraka.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Katibu Mtendaji wa Tume
hiyo Bw.Griffin Mwakapeje wakati akifungua kikao cha wataalamu wa TEHAMA kutoka
Taasisi mbalimbali wakishirikiana na wanasheria
wa Tume hiyo, Mkutano ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume zilizoko
Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mwakapeje ameeleza kwamba mfumo huo utakaojulikana utakapokamilika
utajulikana kwa jina la Law Reform Management Information System
(LRMIS) utasaidia kurahisisha Mtiririko wa utendaji kazi (Business process), kufanya
tathmini mbalimbali zitakazosaidia kubaini idadi ya mapendekezo ya Tume
yaliyutumika katika maboresho au kuunda sheria mpya na utapunguza gharama
wakati wa kuandika maandiko mbalimbali
“serikali imeridhia Uwepo wa mfumo huo na ni ukweli kwamba
utawasaidia sana watafiti wetu katka utendaji kazi za Mapitio, Tathmini, na
Utafiti wa Sheria mbalimbali i”
Akiongea wakati wa kikao kazi hicho Katibu huyo amewataka
wataalamu hao kuhakikisha mfumo unaweza kuwasiliana au kushirikiana na mifumo
mingine ili dhana ya kurahisha utendaji kazi iweze kupatikana kwa urahisi.
Aidha ameeleza kwamba kwa kutumia mfumo huo utasaidia
kupunguza gharama na muda kwa kuwa utakuwa na uwezo wa kuwasiliana na mifumo
mingine ya Taasisi za Kisheria ikiwemo mifumo ya Wizara ya Katiba na Sheria,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na mifumo ya Mahakama.
Akimalizia hotuba yake Mwakapeje amesema kwamba Tanzania kuna
sheria zaidi ya 450 ambazo wanapaswa kuzifanyia mapatio ili kuona zinaendana na uhalisia
katika mazingira ya sasa huku akibainisha kwamba kuna maeneo mengine mapya ambayo
huibuka kila siku yanayohitaji kutengenezewa sheria.
Kikao hicho kitafanyika kwa muda wa siku kumi (10) na
kitawahusisha wataalamu mbalimbali ambapo mfumo wa Mtiririko wa utendaji kazi (Business
process) uliohuishwa utakuwa umepatikana pamoja na mahitaji mengine ya mfumo.
Mwisho
No comments: