Wakili wa Serikali kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Ismail Hatibu (kushoto) akimsikiliza kwa makini David Evance Komba Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Cha Katoliki Mbeya wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Nanenane katika viwanja vya mwakanganle vilivyopo mjini Mbeya
Wananchi wakiendelea kumsikiliza
Wadau wa Sheria Mkoani Mbeya wameiomba Serikali kutilia mkazo mapendekezo yanayoletwa na Tume ya Kurekebisha Sheria Nchini ili kuondoa Sheria ambazo zimekuwa za muda mrefu tokea kipindi cha Ukoloni.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wadau hao wamesema zipo sheria ambazo Tume ya Kurekebisha Sheria Nchini walizitolea mapendekezo ikiwemo Sheria nyingi tulizorithi kutoka kwa wakoloni ikiwemo Sheria ya Vizazi na Vifo ya Mwaka 1920 ambayo imepitwa na wakati.
David Evance Komba Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Cha Katoliki Mbeya amesema kuna umuhimu wa kukibadilisha Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria ya mwaka 1980 kubadilishiwa ili kuitaka Serikali iweze kutilia mkazo mapendekezo yanayotolewa na Tume ya Kurekebisha Sheria kwa kuwa yamekwishafanyiwa utafiti wa kutosha.
David aliendelea kueleza kwamba kwa kutumia Sheria zilizopitwa na wakati zinaweza kusababisha hasara kwa serikali na kuleta ukakasi katika upatikanaji wa takwimu huku akitolea mfano Sheria ya Vizazi na Vifo ya mwaka 1920 inavyoweza kutoa nafasi ya kupata cheti cha kuzaliwa au cha kifo zaidi ya mara moja kwa mtu mmoja.
Anasema kupitia Sheria hiyo kumekuwa na udanganyifu wakati wa kutafuta ajira au kuomba mikopo ya elimu ya juu kwa kutumia vyeti hivyo.
No comments: