TIMU ya kuvuta Kamba wanawake kutoka Tume ya Kurekebisha
Sheria Tanzania leo imepoteza tena mchezo wake dhidi ya Wizara ya Utalii huku
wakibainisha kwamba idadi ndogo ya wachezaji walionao imechangia kupoteza mchezo
huo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baada ya
kumalizika kwa mchezo wa kuvuta Kamba uliokuwa ukifanyika katika viwanja vya
Mkwawa mjini Iringa, wachezaji wa timu hiyo
wamesema walijiandaa vizuri lakini walizidiwa nguvu kwa kuwa walikuwa
wachache ikilinganishwa na timu pinzani ambayo ilikuwa na wachezaji 10 huku wao
wakiwa 9.
Hata hivyo walibainisha kwamba wamekuwa
wakicheza pungufu kwa kuwa baadhi ya wachezaji wao walipata majeraha wakati wa
mazoezi na wengine kupata udhuru jambo ambalo lilipunguza nguvu ya timu hiyo.
Aidha wachezaji hao wamewaomba watumishi wa
Tume hiyo na wapenzi wote wa mchezo huo kuwaombea dua ili kupata ushidi katika
mchezo unaofuata kwa kuwa wana mwalimu mzuri nguvu wanazo na mbinu mbalimbali
za kupata ushindi.
Kwa upande wake Mwalimu wa timu hiyo Bw. Idrisa
Juma Shabani alisema timu imejiandaa vizuri changamoto iliyotokea ni kuzidiwa
nguvu na timu pinzania hivyo wanaendelea na mazoezi ili kuukabili mchezo wa unaofuata.







No comments: