Timu ya Kuvuta Kamba wanaume kutoka Tume ya Kurekebisha
Sheria Tanzania leo imeibuka mshindi baada ya kuivuta timu ya RAS Mbeya kwa
ushindi wa 1-0 katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za
Serikali ( SHIMIWI), mchezo uliofanyika katika viwanja vya Mkwawa Mkoani Iringa
.
Katika mchezo wa kwanza timu zote zilimaliza kwa
kutoshana nguvu na baada ya kuanza kwa kipindi cha pili cha mchezo, Tume sheria
Sport Club waliweza kuibuka washindi kwa kuwavuta wapinzani wao katika dakika
ya kwanza na sekunde 34.
Akiongea mara baada ya mchezo huo, Mwalimu Idrisa Juma Shabani wa timu ya Tume sheria Sport Club amewapongeza wachezaji
wake kwa kufuata maelelekezo na kuwataka waendelee kuwa na ari kubwa ya mchezo ili
kuweza kuingia hatua ya robo fainali ingawa tulipoteza mchezo wa jana.
“Tumeshinda lakini mchezo haukuwa mrahisi,
wachezaji wamejituma kwa kiasi kikubwa unaweza kuona awamu ya kwanza tulitoa
droo, tukabadilisha mbinu hatimaye tukapata ushindi,japo haikuwa kazi rahisi”
alisema Mwalimu Idrisa.
Aidha Mwalimu ameelza kwamba mashindano hayo
hayakuwa rahisi kwa kuwa timu zote zimejiandaa vizuri na kila timu ilitaka kujihakikishia
kupata ushindi utakaofanya wasonge mbele katika mashindano hayo huku akibainisha kwamba siri
kubwa ya ushindi walioupata ilikuwa ni umoja na mshikamano
walioutengeneza .
Hata hivyo, ameeleza kwamba bado wameendelea
kuwa na kibarua kigumu ambacho ambapo siku inayofuta watakuwa na mchezo
mwingine mgumu ambao ni lazima washinde ili waweze kuendelea katika hatua ya
robo fainali.
Kwa upande wake mchezaji wa nyuma katika mchezo
huo (stopper) Bwana Japhace Tumaini alipohojiwa
ameeleza kwamba mazoezi waliyoyafanya
jana baada ya kupoteza mchezo wao na Wizara ya fedha yaliwajenga
ikiwa ni pamoja na kubadilisha mbinu za uvutaji walizozipata kupitia kwa
mwalimu wao jambo ambalo lilisababisha ushindi kupatikana.
Bw. Japhace amesema kwamba wanaendelea na
mazoezi kwa lengo la kuhakikisha kwamba wanapata matokeao katika mchezo
unaofuta ili timu iweze kuingia hatua ya nane bora.
Mwisho






No comments: