Utafiti umebainisha kwamba usuluhishi wa makosa dhidi
ya maadili nje ya mfumo wa mahakama
imekuwa ni sababu ya Kuongezeka kwa utendekaji wa makosa hayo kwakuwa Sheria ya Mwenendo
wa Mashauri ya Jinai inaeleza kwamba makosa dhidi ya maadili Tanzania si
miongoni mwa makosa yanayoweza kusuluhishwa nje ya mahakama.
Hayo yamebainishwa
na Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania Jaji Mstaafu January Msofe
wakati akiwasilisha taarifa za mapitio ya mfumo wa sheria zinazosimamia
makosa dhidi ya maadili Tanzania na taarifa ya mapitio ya mfumo wa sheria
zinazosimamia udhamini Tanzania.
Jaji Msofe amesema
kwamba utafiti umebaini kuwa sehemu kubwa ya jamii ya Tanzania inasuluhisha
makosa hayo katika ngazi za familia, taasisi za dini, Serikali za Mitaa au
Mabaraza ya Kata Ingawa
Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai inaeleza bayana kwamba makosa
dhidi ya maadili Tanzania sio miongoni mwa makosa yanayoweza kusuluhishwa nje
ya mahakama.
” sababu
nyingine inayochangia kuongezeka kwa utendekaji wa makosa dhidi ya maadili ni
usuluhishi wa makosa hayo nje ya mfumo wa mahakama. Ingawa Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai
inaeleza bayana kwamba makosa dhidi ya maadili Tanzania si miongoni kwa makosa
yanayoweza kusuluhishwa nje ya mahakama, utafiti umebaini kuwa sehemu kubwa ya
jamii ya Tanzania inasuluhisha makosa hayo katika ngazi za familia, taasisi za
dini, Serikali za Mitaa au Mabaraza ya Kata” Jaji Msofe.
Naye Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Pindi Chana
wakati wa kikao hicho ameipongeza tume hiyo kwa kutekeleza majukumu yake kwa
ufasaha jambo ambalo ameeleza kwamba linachangia kuimarisha Amani na utulivu
nchini.
Aidha amewataka Watanzania kutumia madawati
maalumu ya huduma ya msaada wa sheria unaotolewa katika ngazi za kata Wilaya na
Mkoa ili wapate elimu na waweze kutatua changamoto zinazowakabili huku
wakitakiwa kutokuwa waoga kuomba kuelimishwa kuhusu changamoto zinazowakabili
na namna ya kuzitatua.






No comments: