KATIBU Tawala Mkoa wa Rukwa Gerald Kusaya ameipongeza Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT)
kwa uamuzi wake wa kutoa elimu kuhusu sheria mbalimbali Katika shule za msingi na sekondari Mkoani
hapo kwa na lengo la kuongeza uelewa wa sheria na utii wa sheria bila shuruti.
Ametoa pongezi hizo leo tarehe 21/11/2023 ofsini kwake baada
ya kukutana na ujumbe kutoka Tume hiyo ambao walimfahamisha kwamba wapo Mkoani
hapo kwa lengo la kutoa elimu ya sheria
kwa wanafunzi wa shule za msingi na
Sekondari.
Bwana Kusaya amesema zoezi hilo litakuwa na tija kubwa kwa jamii kwa kuwa jamii ina
uhitaji mkubwa wa elimu ya sheria. Aidha, ameeleza kwamba elimu hiyo itawasaidia watoto kufahamu haki
na wajibu wao na kujiepusha kutenda makosa mbalimbali yaliyoanishwa katika
sheria husika.
" Niwapongeze kwa uamuzi wa kutembelea wanafunzi na
kuwapa elimu ili watambue haki na wajibu wao katika jamii, kwa kweli huduma
yenu inahitajika sana Mkoani hapa" alisema Kusaya.
Aidha, Katibu Tawala huyo ameiomba Tume ya Kurekebisha
Sheria kuendelea kutoa elimu hiyo kwenye
shule na vikundi mbali mbali vya vijana na wajasiriamali kwa kuwa uelewa wa
sheria utasaidia wananchi kutii sheria bila shuruti.
Hata hivyo Kusaya ameshauri elimu hiyo kuendelea kutolewa
katika makundi mbalimbali ya jamii na bila kusuburi watende makosa na
kufikishwa mahakamani.
Awali akitoa maelezo ya utambulisho Mkuu wa Kitengo Cha Elimu ya Sheria kwa Umma, Naibu Katibu
Mtendaji, Bi Zainabu Chanzi amesema miongoni mwa majukumu ya Tume hiyo ni kutoa
elimu kwa umma ili kuisaidia jamii kuzielewa Sheria mbalimbali na kupunguza
utendekeji wa makosa mbalimbali ya
jinai.
Elimu iliyotolewa ni kuhusu Sheria ya Mtoto,Makosa dhidi ya
Maadili ya Utu,Makosa ya Kimtandao, Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za
Kulevya, Ziara hiyo itachukua muda wa siku mbili na shule mbalimbali za Manispaa
ya Rukwa zipata huduma hiyo.






No comments: