HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

» » » TUME YA KUREKEBISHA SHERIA WAJIPANGA KUTOA ELIMU KWA WAKURUGENZI WA HALMASHURI

 


























Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) imejipanga kutoa elimu ya Sheria kwa Wakurugenzi na Wakuu wa Idara Katika Halmashauri mbalimbali hapa nchini ili kuongeza uelewa juu ya mabadiliko mbalimbali katika sheria .


Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Zainabu Chanzi  alipokuwa akijibu maombi ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Mifugo katika Halmashauri hiyo, Bw. Tilinao Nsila.


Naibu Katibu  alieleza kwamba moja ya majukumu ya Tume ya Kurekebisha Sheria  ni kutoa elimu ya sheria hivyo utekelezaji wa ombi hilo utaanza mara moja kuzingatia  bajeti pamoja na majukumu mengine ya Tume.


Aidha, Naibu katibu alibainisha kwamba  wakurugenzi na watumishi wengine ni wadau muhimu  hasa katika kipindi hiki ambacho Taasisi inaendelea kukusanya maoni kwa ajili ya maboresho ya sheria mbalimbali.


"Katika Halmashauri zetu Wakurugenzi ni wasimamizi muhimu wa Sheria hivyo inafaa wapewe elimu kuhusu utekelezaji wa sheria mbalimbali  ili   kupunguza utendekaji wa makosa katika Jamii" alisema Naibu Katibu Zainabu.


Awali, Kaimu Mkurugenzi huyo alieleza kwamba sheria zinafanyiwa maboresho mara kwa mara  na kuna baadhi ya sheria ambazo hazifahamiki kwa watu na viongozi ambao ndio wanaosimamia utekelezaji wa sheria na maendeleo ya wananchi katika ngazi za Halmashauri.


" Naomba elimu ya mabadiliko ya Sheria mbalimbali zitolewe kwa Wakurugenzi na wakuu wa Idara kwa kuwa itasaidia utoaji wa huduma kwa jamii kwa kufuata sheria"


Katika  mkoa wa Katavi wataalam kutoka Tume hiyo walitoa elimu ya sheria ya makosa dhidi ya maadili,Sheria ya Kudhibiti  na  Kupambana na Dawa ya Kulevya, Makosa ya Kimtandao na Utakasishaji wa Fedha Haramu. Mafunzo hayo yalitolewa katika chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Mpanda, Chuo cha Sayansi na Maendeleo ya Jamii Mpanda,  vikundi vya waendesha bodaboda na bajaji, viongozi wa dini watendaji wa kata na wanawake wajasiriamali.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Tuandikie Maoni yako