Kamati ya
Bajeti ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania leo imekutana Jijini Arusha
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Hazina Ndogo kwa lengo la kuandaa Mpango na Bajeti ya Tume kwa
mwaka wa fedha 2024/25 ambao utasaidia
kuendesha shughuli za Taasisi hiyo.
Akiongea katika ufunguzi wa Kamati hiyo Naibu Katibu
kwa niaba ya Katibu Mtendaji, Bw.Burhani Kishenyi amesema Mpango na Bajeti
ujielekeze katika kuimarisha shughuli za mapitio, tathmini, utafiti na elimu ya
sheria kwa umma kwa kuzingatia Mpango wa Maboresho ya Sheria na utekelezaji wa masuala ya Haki Jinai.
Bw. Kishenyi ameeleza kwamba utekelezaji wa Mpango na Bajeti ni muhimu ukajielekeza katika
matumizi ya TEHAMA pamoja na kuendeleza rasilimali watu kwa kuwajengea uwezo
watumishi kwenye mafunzo ya muda mfupi na mrefu.
Aidha ameeleza kwamba utekelezaji wa Mpango na Bajeti
utajielekeza kwenye matumizi ya mifumo mbalimbali ikiwemo Mfumo wa manunuzi (NeST) na Mfumo wa Kupima Utendaji Kazi wa
Watumishi wa Umma na Taasisi ( PEPMIS).
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mipango
na Uratibu Bi. Fatma Alawi amesema kikao hicho kitasaidia kuwajengea uwezo maafisa
wa bajeti katika usimamizi na ufuatiliaji wa kazi.







No comments: