Wakuu wa Vitengo wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT)
wametakiwa kujifunza mifumo yote ambayo Serikali inaitumia katika utekelezaji wa
shughuli zake ikiwemo mfumo wa manunuzi (NEST, ESS) kwa kuwa Serikali imehamia
kwenye mifumo ya kielekitroniki.
Maelekezo hayo yametolewa
leo tarehe 9/01/2024 na Katibu
Mtendaji wa Tume hiyo George Mandepo
wakati wa kikao cha Menejimenti kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano
wa ofisi hizo ambapo aliagiza kila Mkuu wa Kitengo kujifunza mifumo
iliyoandaliwa na Serikali ili kusaidia utekelezaji wa shughuli za kila siku
zikiwemo za manunuzi.
“kila mkuu wa kitengo
ahakikishe anajifunza mifumo iliyopo ili asikwame kutoa huduma, Serikali
imehamia kwenye utumiaji wa mifumo ya elekitroniki ambapo huwezi kununua
chochote nje ya mfumo, na utekelezaji wa majukumu yetu unategema mifumo hiyo. ”
George Mandepo.
Katibu Mtendaji ameelekeza kutafutwa wataalamu wa mifumo
ambao watatoa mafunzo kwa watumishi wote wa Tume kwa wakati ili kuboresha
utendaji kazi.
Hata hivyo ameelekeza kamati za mafunzo kutekeleza majukumu yake kwa kutoa mafunzo maalumu kwa madereva ikiwa ni pamoja
na elimu ya utambuzi pindi panapokuwa na magari mapya ya ofsini.
Aidha, amewataka
watumishi kujenga utamaduni wa kutunza vitendea kazi yakiwemo magari huku
akitaka akiwakumbusha madereva kutii
sheria za barabarani bila shuruti ili kuepusha ajali na uharibifu wa mali za serikali.
Mwisho






No comments: