HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

» » WATUMISHI TUMESHERIA WAHIMIZWA KUANDIKA TAARIFA WANAPORUDI KUSHIRIKI MAFUNZO AMA KUSAFIRI NJE YA KITUO CHA KAZI.

 

 










Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wametakiwa kujenga mazoea ya kuandika taarifa baada ya kukamilisha kazi na baada ya kumaliza Mafunzo kwa  wanaohudhuria  ili kujenga uelewa wa pamoja Katika Taasisi.

 Maelekezo hayo yametolewa na Kaimu Katibu Mtendaji Tume hiyo Burhan Kishenyi Leo tarehe 06/12/2023 wakati wa Kikao Cha watumishi wote kilichofanyika Katika ukumbi wa mikutano ofsini hapo ambapo alieleza umuhimu wa kuandika taarifa kwa kila kazi au Mafunzo atakayopata mtu ili kutengeneza kumbukumbu za Taasisi na kuwa na uelewa wa pamoja.

 

"Wapo watu wanaenda  Mafunzo ya muda mfupi na mrefu na wengine wakiwa wanasafiri sehemu mbalimbali kwa ajili ya kufanya kazi lakini wakirejea Ofisini hawaandiki taarifa ya walichojifunza  (back to office report).

 

Aidha amehimiza kila mtumishi ambaye  atakwenda safari ya kikazi au Mafunzo ndani na nje ya nchi au vikao vya nje ya ofisi wanapaswa kuandika taarifa kueleza yaliojiri  na kuonesha mapendekezo kulingana na changamoto zilizojitokeza.

 

Kwa upande wake Naibu Katibu Mtendaji Zainab Chanzi, amewataka watumishi hao kuongeza juhudi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wenye ujuzi ili kuweza kuhamishia ujuzi kutoka mtumishi mmoja hadi mwingine.

 Akitolea mfano wa Mafunzo ya mifumo mbalimbali amesema kila mtumishi anatakiwa kujua mifumo unavyofanya kazi hivyo watumishi wanatakiwa kuwa tayari kujifunza kupiatia  kwa wenzao hasa Katika kipindi hiki ambapo serikali inafanya kazi kidijitali.

 Naye Mwansheria Mwandamizi Dkt kalekwa ameishauri Tume hiyo Kuwekeza kwenye elimu  ili kupata viwango vya uzamivu ( hard skills )na uwezo au mbinu za kutumia taaluma hizo ( Soft skill).

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Tuandikie Maoni yako