Katibu
Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. George Mandepo amewataka wadau wa sheria nchini kuwasilisha maoni yao juu
ya sheria mbalimbali kwa Serikali kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria na Tume
itayafanyia kazi kwa kuzingatia taratibu
zilizowekwa.
Bw.
Mandepo ameeleza hayo leo tarehe 7 Februari 2024 jijini Dodoma wakati wa kufanyia
tathmini ya maoni ya baadhi ya wananchi
waliyoyatoa wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyomalizika tarehe 1 Februari
2024 na kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassani ambapo wananchi wengi waliomba Tume ya Kurekebisha Sheria kuwatembelea
maeneo yao ili kupata maoni yao kuhusu utekelezaji wa sheria mbalimbali hapa
nchini.
Katibu
huyo alisema kwamba, Tume ya Kurekebisha imekuwa ikikutana na wadau mbalimbali katika
utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku na wakati wa kufanya utafiti na utoaji
wa elimu ya sheria kwa umma ambapo ameeleza kwamba, kupitia utaratibu huo mwananchi mojamoja au vikundi wamekuwa wakipata fursa ya kutuoa maoni yao kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia barua pepe (E-mail), barua ya kawaida,
kupiga simu au kuonaa moja kwa moja na Maafisa husika wa Tume ili kueleza changamoto wanazoziona katika sheria zilizopo
au mapungufu yoyote kwenye utendaji ambayo wanadhani yanahitaji kuwekewa mfumo
wa sheria.
“Tumekuwa
tukikutana na wananchi wakati wa utafiti , kutoa elimu kwa umma na wakati wa
tathmini lakini bado wananchi wanaweza kutuandikia, kutupigia simu au
kutembelea ofisi zetu na kutoa maoni yao na tutatapokea na kuyafanyia kazi kwa
kuzingatia taratibu zilizowekwa”
Aidha,
akitolea ufafanuzi swali la mwananchi mmoja aliyeomba Tume itembelee mahabusu
na ikiwezekana wanasheria wakakae magererezani kama wafungwa ili waweze kuviona
vipengele vya sheria vinavyostahili kubadilishwa (https://youtu.be/7HEO1Amp-
yenye kichwa cha habari ‘Nendeni magerezani/Mhabusu huko mtaona
vipengele vya kurekebisha”. Bw. Mandepo amesema kuwa, Idara ya Magereza
ni moja ya mdau muhimu wa Tume na Magereza
ni eneo mojawapo la kupata taarifa za kitafiti zitakazosaidia pia kufanya marekabissho ya sheria kama pia
ilivyowahi kupendekezwa na Tume ya Haki Jinai. Alibainisha kuwa, kwa sasa
Serikali inafanyia kazi mapendekezo ya mapitio ya sheria mbalimbali
zinazosimamia haki ikiwemo zile zinazohusisha haki jinai.






No comments: