HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

UTAFITI NI NJIA YA UHAKIKA YA KUWEZESHA KUWA NA SHERIA MADHUBUTI NA ZENYE TIJA KWA TAIFA- MANDEPO

 


Katibu Mtendaji Tume ya Kufekebisha Sheria Tanzania Bw. George Nathaniel Mandepo amesema kuwa utafiti ni mbinu  muhimu inayoweza kusaidia Serikali  kuamua kama sheria au iboreshwe au ifutwe ili kuendana na mahitaji halisi ya  Taifa kwa wakati husika. 

Akizungumza katika kipindi cha Morning Trumpet cha Azam Tv kinachorushwa kila siku asubuhi kiliendesha mahojiano  kuhusu maendeleo ya sheria nchini, ambapo Bw. Mandepo alisema kuwa jamii inapobadilika, ni lazima sheria nazo zibadilike kulingana na hali. Mabadiliko hayo uhususha pia matokeo ya tafiti mbalimbali za Sheria zinazofanywa na Serikali  hususan kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. 

“Utafiti ndio unaoamua kwamba sheria itungwe, ifutwe au iboreshwe,” alisema Mandepo huku akisisitiza umuhimu wa kuihusisha Tume hiyo katika michakato muhimu ya maboresho ya sheria hapa nchini.

Alieleza kuwa tafiti husaidia kubaini changamoto zilizopo kwenye sekta husika na pia ni mbinu ambayo uhusisha  wananchi wanaweza kuguswa au kuathirika kutokana na uwepo au kukosekana kwa sheria katika mbalimbali sekta kama elimu, afya, usalama barabarani na teknolojia. Utafiti hutoa  mwanga kwa watunga sheria kuchukua hatua sahihi, yenye tija na husishi. 

Kwa mujibu wa Mandepo, baadhi ya sheria zimekuwa zikiboreshwa kutokana na mabadiliko ya kijamii na maendeleo ya sayansi na teknolojia hapa nchini.  

Alitoa mfano wa sheria za mawasiliano na matumizi ya mitandao ambazo zimekuwa zikifanyiwa marekebisho mara kwa mara kutokana na ukuaji wa teknolojia duniani.
Mathalani kwa sasa amesema,kwa maelekezo ya Serukali, Tume  hiyo  inaendelea na kazi ya utafiti wa mifumo ya sheria zinazoratibu matumizi ya Akili Ude (Artificial Intelligence ) na utatifi wa mifumo ya Sheria zinaohusu Biashara ya  Hewa Ukaa. 

Kadhalika, alieleza kuwa, miongoni mwa kazi ambazo Tume hiyo imefanya hivi karibuni ni Tathmini na Mapitio sheria za Michezo ya Kubahatisha, Sheria ya Takwimu, Sheria ya Vyama vya Ushirika, Ulinzi Mashahidi na Watoa Taarifa, Matumizi ya Shisha, Bidhaa za Tumbaku na Sigara za Kielektroniki, Sheria ya Usuluhishi  pamoja na Sheria ya Makampuni na Majina ya Biashara. Pia mapendekezo ya kuboresha Sheria yametolewa kwenye Sheria za Usafirishaji Majini na Ardhini.

Aliainisha kuwa kwenye eneo ya haki jinai, Tume hiyo imepitia na kutoa mapendekezo juu ya maboresho ya sheria kwq kuzingatia matokeo ya Tume ya Rais ya Kuangalia Mifumo ya Haki Jinai (Tume ya Hakijinai). Baadhi ya Sheria zilizotazamwa ni pamoja na Sheria za Mwenendo wa Jinai, Sheria zinazogusa dhamana na Sheria ya Uhujumu Uchumi na Uharifu wa Kupangwa. 

Alisisitiza kuwa, kutokea kuanzishwa kwake, Tume imeweza kufanya Tafiti, Tathmini na mapitio ya Mifumo ya Sheria mbalimbali na kutoa Taarifa zaidi ya 70 zilizowezesha Serikali kuboresha sekta husika kwa kutunga, kufuta au kufanya mabadiliko kwenye sheria nyingi zinazogusa nyanja za haki madai na haki jinai, ajira, mahusiano, kazi,  jamii, siasa, uchumi na maendeleo ikiwemo vivutio vya uwekezaji, mifumo ya utatuzi wa migogoro na kodi. 

Tume hiyo imeendelea kutoa Elimu kwa Umma kuhusu sheria mbalimbali kwa nia ya kuwezesha wadau kufahamu haki na wajibu wao ndani ya sheria zilizopo. 

Aidha, wadau wametakiwa kushiriki katika tafiti, tathmiji na mapitio ya sheria na kutoa maoni yao ili kusaidia kujenga sheria bora zinazolinda haki, usawa na maendeleo ya taifa.

SERIKALI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA 2025/2026 YA LRCT- NAIBU WAZIRI.

 


  • Naibu waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Zainabu Katimba akiongea na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kwenye Ukumbi wa mikutano wa Tume ya Utumishi wa  Mahakama ulioko Dodoma wakati wa Baraza la wafanyakazi  la Tume hiyo.

  • Naibu waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Zainabu Katimba amesema Serikali inaridhishwa na utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ambapo imeendelea kufanya tafiti na mapitio ya sheria mbalimbali pamoja na kutoa elimu ya sheria kwa umma.

    Kauli hiyo ameitoa tarehe 14/05/2026 katika ukumbi wa mikutano wa Tume ya Utumishi wa Mahakama uliopo mjini Dodoma wakati wa kikao cha 24 cha Baraza la wafanyakazi wa Tume hiyo ambapo ameeleza kwamba Tume imefanya mapitio ya sheria muhimu zikiwemo Sheria ya Usuluhishi, Sura ya 15; Sheria ya Bima, Sura ya 394; na Sheria ya Bima za Vyombo vya Moto (Magari) Sura ya 169, kwa lengo la kuhakikisha zinaendana na mahitaji ya sasa ya kijamii na kiuchumi.

    Mhe. Katimba alifafanua kwamba Tume inaendelea na mapitio ya Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, Sura ya 295, Tathmini ya utekelezaji wa sheria zinazohusu umiliki wa mali na rasilimali asilia pamoja na kufanya tafiti katika maeneo mapya kama matumizi ya Akili Unde (Artificial Intelligence), biashara ya hewa ya ukaa, adhabu ya kifo na kifungo cha maisha, na usajili wa mawakili.

    “Hatua hizi zinaonesha mchango mkubwa wa Tume katika kusaidia Serikali kuwa na sheria zinazoendana na mabadiliko ya teknolojia, uchumi na mahitaji ya wakati” alieleza Mhe. Katimba.

    “Ninapenda kutambua kwa heshima kubwa juhudi zinazoendelea kufanywa na Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania katika kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuishauri Serikali kuhusu maboresho ya sheria mbalimbali kwa ajili ya kuendana na mahitaji ya wakati na maendeleo ya Taifa letu” Aliendelea Kusema.

    Aidha Katika mwaka wa fedha 2025/2026, Tume imewasilisha taarifa tano (5) kwa waziri wa katiba na Sheria ambazo ni Taarifa ya Mapitio ya Sheria ya Takwimu, Sura ya 351 na Taarifa kuhusu Utafiti wa Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Vyama vya Ushirika, za Februari,2025; Taarifa ya Mapitio ya Sheria Zinazosimamia Udhibiti wa Matumizi ya Bidhaa za Tumbaku, Shisha na Sigara za Kielektroniki, Taarifa ya Tathimini ya Utekelezaji wa Sheria ya Michezo ya Kubahatisha Nchini, Sura ya 41 na Taarifa ya Utafiti kuhusu Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Utatuzi wa Migogoro ya Mikopo katika Benki na Taasisi za Fedha, zote za Julai, 2025.

    Awali akimkaribisha Waziri huyo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. George Mandepo alisema Mkutano huo utakuwa na mada zitakazo wasilishwa kwa lengo kuongeza uelewa wa shughuli za Tume, kukuza ujuzi na uzoefu katika kuimarisha utendaji kazi ambazo ni Mada kuhusu ukamilishwaji wa Mpango Mkakati wa Tume wa miaka mitano 2026/2027 – 2030/2031; Mada kuhusu Elimu ya usimamizi wa Fedha (Financial Literacy); na Mada kuhusu Maana ya Maadili na Umuhimu wa Uadilifu katika Utumishi wa Umma.

    Aidha Bw. Mandepo alieleza kuwa mwaka wa fedha 2025/2026, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania iliidhinishiwa na Bunge kutumia jumla ya Shilingi bilion 7.45 Kati ya fedha hizo, kiasi cha Shilingi bilion 1.775 ikiwa ni kwa ajili ya Mishahara na kiasi cha Shilingi bilion 5,627 ikiwa ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo.

Elimu ya Sheria kwa watanzania ndio Mpango mzima

Mtazamo wa Jaji Winifrida Korosso kufuatia Maadhimisho ya wiki ya Sheria

Mabaraza ya wafanyakazi yatumike Kujenga Demokrasia sehemu za kazi - Kabudi



Mabaraza ya  wafanyakazi yanapaswa kutumika kama chombo muhimu katika kuboresha na kuimarisha demokrasia kwenye eneo la kazi badala ya kutumika pekee kukusanya na  kupitia maoni ya watumishi .


Kauli hiyo imetolewa tarehe 14/11/2024 na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Midland iliyopo mjini Dodoma wakati akifungua kikao cha 21 cha baraza la wafanyakazi la Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ambapo ameleleza mabaraza hayo  yanahusisha ushirikishwaji wa wafanyakazi katika maamuzi ya Taasisi au shirika wanamofanyia kazi jambo ambalo  huongeza uwazi na uwajibikaji.

Waziri Kabudi ameipongeza Manejimenti ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kwa kutimiza takwa la kisheria la kufanya kikao cha baraza huku akifafanua kwamba Baraza la Wafanyakazi halipaswi kuwa chombo cha kupokea malalamiko ya watumishi pekee ingawa ni muhimu kwa baraza hilo kushughulikia malalamiko na changamoto zinazowakabili wafanyakazi na badala yake  jukumu lake linapaswa kuwa pana zaidi. 

Prof amefafanua kwamba Baraza linaweza na linapaswa kuwa jukwaa la kuchochea maendeleo, kutoa maoni, na kutoa mawazo ya kuboresha ufanisi wa Taasisi kwa ujumla.

Demokrasia  katika eneo la kazi ni muhimu kwani inachochea ari ya kazi, kuimarisha ufanisi, na kujenga mazingira yenye amani na haki, alisistiza Waziri wa Kabudi.

“ Baraza la Wafanyakazi si tu chombo cha kusimamia haki za wafanyakazi, bali pia ni nyenzo muhimu ya kufanikisha malengo ya taasisi kupitia ushirikiano wa kweli na mawasiliano ya wazi” alisema Waziri 

Amesema  Baraza linatoa nafasi kwa wafanyakazi kutoa maoni, mawazo, na mapendekezo kuhusu masuala yanayohusu ustawi wao na maendeleo ya Taasisi kwa ujumla  hivyo kupitia Baraza la Wafanyakazi, viongozi watakiwa  kupata mawazo mapya ya kuboresha mazingira ya kazi.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Bw. George Mandepo, alieleza kwamba kikao hicho ni hitaji la kisheria na ni muhimu kwa kuwa linashirikisha  wafanyakazi katika michakato ya kufanya maamuzi ili kuimarisha ufanisi wa kazi.


Aidha amefafanua kwamba Tume inatekeleza mipango mbalimbali ya kuhakikisha kwamba watumishi wanapata mafunzo  ili kuwajengea uwezo na kuboresha ufanisi  katika kutekeleza majukumu yao.

Mkutano huo uliwaleta pamoja wafanyakazi wa Tume na wadau wengine muhimu kwa lengo la kujadili masuala ya kazi, kubadilishana mawazo, na kutafuta suluhisho la changamoto zinazokabili sekta ya sheria.


MWISHO

WAASISI WALIVYO ELEZEA HISTORIA YA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA

SIKILIZA: PAMBAZUKO NA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA

Elimu Ya Sheria Ya “Plea Bargaining" Ilivyofungua Vichwa Vya Wakazi Wa Mkoa wa Arusha

 




Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) imefanya ziara katika Mikoa ya Manyara, Arusha  na Kilimanjaro kwa lengo la kutoa elimu ya sheria mbalimbali kwa wananchi

Ziara hiyo ilibainisha kwamba Sheria ya “plea bargaining” imeleta mwamko mkubwa miongoni mwa wakazi wa Mkoa wa Arusha na kwingineko Tanzania kutokana na manufaa yake ya kupunguza muda wa kesi, gharama za uendeshaji wa mashauri, na hata kuepuka msongamano katika magereza.

Hayo ni baadhi mambo ambayo wananchi mkoani Arusha walizungumza kwa njia ya simu na ujumbe mfupi wa maneno katika kituo cha Redio cha TBC na Savvy Fm wakati Wanasheria wa Tume hiyo Vick Mbunde na Anjela Shila wakitoa elimu ya sheria  kuhusu kupunguziwa adhabu kwa kukiri kosa.

Awali akifafanua kuhusu sheria hiyo Wakili wa Serikali Vicky Mbunde alisema kwamba  Plea bargaining, inayojulikana pia kama makubaliano ya kukiri kosa kwa makubaliano maalum, sheria ambayo ilianza kutumika rasmi Tanzania kupitia mabadiliko ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) ya mwaka 2019, na imekuwa ikihamasishwa kwa nguvu katika mfumo wa sheria.

“mtuhumiwa anapokiri kosa mbele ya muendesha mashtaka , anaweza kupunguziwa adhabu baada yay a mahakama kujiriidhisha na alichokiri . Huu ni utaratibu unaotambuliwa kisheria kama "plea bargaining" ambapo mahakama inaweza kuzingatia kukiri huku kama sababu ya kupunguza adhabu”. Alisema Wakili Vicky Mbunde.

Katika kipindi hicho ambacho wananchi wengi walipiga simu na kutuma ujumbe ,fupi waliuliza idadi kubwa ya maswali huku wakitwataka mawakili hao wa serikali kufafanua umuhimu wa kukikri kosa kwa m,mtuhumiwa na upande wa serikali.


Akiji maswali hayo wakili Anjela shila alifafanua kwamba sheria ya Plea Bargaining  ina umuhimu mkobwa kwa wananchi na serikali kwa ujumla kwa sababu inaharakisha  Utaratibu wa Kesi Mahakamani kutokana na idadi kubwa ya kesi zinazojazana kwenye mahakama za ngazi tofauti hivyo , mfumo wa plea bargaining umeonekana kuwa mkombozi kwa kuwa unaruhusu kesi kumalizwa haraka bila kupitia mchakato mrefu wa usikilizaji.

Hata hivyo Wakili Anjela amefafanua kwamba  mfumo huo unasaidia kupunguza Msongamano wa Magereza kwa maana kwamba kuna nafasi ya kuangalia mashauri yao kwa mtazamo mpya, wakati mwingine kupokea adhabu nyepesi kwa kukiri mapema na kupunguza athari za kifungo kirefu bila ulazima ambapo alieleza kwamba mfumo huu pia unahimiza wahusika kubadilika na kujifunza kutoka kwenye makosa bila adhabu kali zisizo za lazima.

Aidha alieleza kwamba mfumo huo unasaidia  kukuza Uwajibikaji na Haki ambapo Kupitia plea bargaining, mahakama na waendesha mashitaka wanaweza kutoa nafasi kwa washtakiwa ambao wako tayari kukiri kosa na kushirikiana na vyombo vya dola kwa uwazi ambao ambalo limeelezewa kwamba linachochea utamaduni wa kuwajibika na kuleta ustawi kwa jamii kwa ujumla.

Hata hivyo Anjela Shila aliongeza kwamba mfumo huo wa sheria una manufaa kwa Wakati wa Uchumi Mgumu ambapo kutokana na changamoto za kiuchumi, plea bargaining imekuwa muhimu kwa kuwa inapunguza gharama kwa pande zote.

Alieleza kwamba serikali inapunguza gharama za  uendeshaji wa kesi ndefu, na kwa washtakiwa, wanapunguza muda wa kutumia kwenye kesi na kufungua nafasi ya kuendelea na shughuli za kiuchumi.

Kulingana na ujumbe na simu zilizokuwa zikipokelewa katika vituo hoivyo vya Redio vinadhibitisha kwamba Wakazi wa Arusha wameanza kuelewa kuwa mfumo huo unaweza kusaidia kupunguza muda wanaotumia mahakamani, jambo ambalo limepunguza shaka na kuleta matumaini kwa wale waliokuwa wakisubiri mashauri yao kwa muda mrefu.