HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

HABARI

» » BILIONI 24.68 KUJENGA OFISI ZA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA LRCT MJI WA SERIKALI DODOMA.

 BILIONI 24.68 KUJENGA OFISI ZA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA LRCT MJI WA SERIKALI DODOMA.









Tume ya kurekebisha sheria Tanzania LRCT imeingia mkataba wa ujenzi wa jengo la ofisi za Taasisi hiyo na kampuni ya Lijun Development Construction Co. Ltd chini ya usimamizi wa wakala wa ujenzi Tanzania (TBA).


Zoezi hilo limefaniyika Novemba 29,2023 Mkoani Dodoma ambapo kazi hiyo imehusisha kutembelea eneo la mradi wa ujenzi huo mji wa serikali Mtumba, ikiwa ni Pamoja na kufanya kikao cha Pamoja kujadili hatua za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo.

Akiongea wakati wa  kikao hicho mkadiriaji majengo( quantity surveyor) kutoka wakala wa majengo Neema Kifua amemtaka mkandarasi kuhakikisha anakamilisha kazi kwa wakati na kufuata mchoro kama mkataba unavyoelekeza.

Aidha amemuagiza mkandarasi kutumia  siku 14 za mwanzo vizuri katika kusafisha eneo na kukusanya vitendea kazi ( mobilization ) ikiwa ni pamoja na kukamilisha taratibu za kukutana na taasis nyingine zinazohusiana na kazi za ujenzi ikiwemo OSHA, Mipango miji na wengine.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Burhani Kishenyi ameziomba pande zote za mradi huo akiwemo fundi mshauri mhandisi muelekezi na mkandarasi kutimiza wajibu wake ili kupunguza changamoto ambazo zinaweza kutokea wakati wa utekelezaji wa majukumu.

Hata hivyo Kishenyi aliomba kuimarishwa kwa njia za utoaji wa faarifa na mawasiliano kwa ujumla ili kuepusha ucheleweshwaji wa kazi kwa vitu ambavyo vingeweza kutatuliwa kwa njia za mawasiliano. 

Ujenzi wa ofisi za Tume ya kurekebisha sheria Tanzania LRCT unatajwa kuwa na thamani ya shilingi za kitanzania 24,680,651,572.45 ( Bilioni ishirini na nne, milioni mia sita themanini, laki sita Hamsini na moja elfu mia tano sabini na mbili na senti arobaini na tano.) ambapo kwa mujibu wa makubaliano ujenzi huo utafanywa katika kipindi cha miezi 24 hadi kukamilika kwake kuanza tarehe 14 mwezi Desemba 2023 hadi mwezi desemba mwaka 2025.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Tuandikie Maoni yako