Mafunzo dhidi ya Afya ya akili na mfuko wa fidia
kwa watumishi (WCF) yametolewa kwa
watumishi wa Tume ya Kurekebisha Tanzania ili kuwajengea uwezo na kuboresha
utendaji kazi wao.
Mafunzo hayo yametolewa leo tarehe 06/12/2023 Katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Tume hiyo ambayo yamehusha watumishi wote ambapo ilielezwa kwamba
Mafunzo hayo yatasaidia watumishi kujua haki zao na namna Serikali inavyoweza
kufidia wakipata ulemavu wakiwa Kazini.
Aidha Mafunzo hayo pia yametajwa kusaidia kuboresha
afya ya akili na vinavyotakiwa kuepukwa
Katika kuboresha afya hiyo.
Awali akiwakaribisha watoa mada hao Naibu Katibu
Mtendaji Burhani Kishenyi amesema kwamba Tume ya kurekebisha sheria Tanzania
imewaalika wataalamu hao ili watumishi watambue haki zao na Kama sehemu ya
kutatua changamoto zinazotokana na ajali Kazini pamoja na matatizo
yanayosababishwa na Afya ya Akili.
Kwa mujibu wa mtaalamu kutoka Taasisi ya Afya ya akili
Milembe Rose Mwangoka amesema Magonjwa ya akili yaliotawala sana kwa sasa ni
pamoja na Msongo wa Mawazo, Sonona,Wasiwasi, Matumizi mabovu ya Vilevi pamoja
na Skizofrenia ambapo ameeleza husabishwa na matatizo ya kibaolojia,
kisaikolojia na kijamii au mazingira.
Akieleza zaidi Rose amesema ili kukabiliana na
changamoto hizo namna sahihi ya kujikinga ni pamoja na kupata muda wa kutosha
wa kulala, kupenda kushirikisha mtu unaemuamini pindi unapokabiliwa na
changamoto pamoja na kupata muda wa kufanya mazoezi ya mwili ili kuimarisha
Afya.
No comments: