Watumishi wa Tume
ya kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) wametakiwa kuzilinda na kutunza Rasilimali zilizopo chini ya Taasisi hiyo
kwa kuwa ndizo zitakazo saidia kuyafikia malengo waliyojiwekea.
Akiongea wakati
wa kikao cha menejimenti ya Taasisi hiyo kilichofanyika Desemba 4, 2023, katika
moja ya kumbi wa mikutano wa ofisi hiyo, Kaimu Katibu Mtendaji Burhani Kishenyi
amesema watumishi wanatakiwa kuzilinda na kuzitunza rasilimali zilizopo ikiwemo,
rasililimali fedha, watu, na rasilimali muda kwa kuwa ndio vitu muhimu katika
kuyafikia malengo waliojiwekea kupitia kazi za kila siku wanazozitekeleza.
“wapo
watumishi ambao wanaacha feni na taa zikiwa zinawaka masaa yote ya kazi, kuanzia
juma tatu hadi juma pili bila kuzimwa jambo ambalo linaongeza gharama za
uendeshaji hii sio sawa lazima kila mtu awe makini na ofisi yake , ofisi ya
utumishi na rasilimali watu waonyeni na ikibidi warudisheni watako acha taa au
feni zikiwaka ofisini kwao hata kama ni muda usiokuwa wa kazi”Kishenyi .
Aidha ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa watumishi
watakaobainika kutumia rasilimali vibaya ikiwemo ofisi, magari na muda na ikiwemo kuwarudisha ofini kuzima taa au feni
watakao bainika kuacha ofisi za katika mazingira hayo hata kama ni siku au muda
usikuwa wa kazi.






No comments: